LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia kuondoa kero ya foleni Dar

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea na mchakato wake wa kufanya maboresho na kuhakikisha kila sehemu yenye kasoro inayoonekana kukwamisha jitihada za kuleta maendeleo nchini, inarekebishwa ili kuleta maendeleo na kuinua uchumi wa nchi.

Jitihada za Rais Samia katika kufanya mabadiliko katika kipindi cha miaka mitatu tangu aingie madarakani, zimeonekana katika sekta mbalimbali ambapo kwa upande wa miundombinu, Rais anaendelea na miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara kwa viwango vya lami na changarawe pamoja na ujenzi wa madaraja makubwa na madogo yakiwemo ya mawe.

Kwa hapa nchini Tanzania, Jiji la Dar es Salaam ndio jiji kubwa kibiashara ambalo lina idadi kubwa ya watu 8,161,230 ongezeko la asilimia 4.95 kutoka mwaka 2023 ambapo ilikuwa watu 7,776,000 na linategemewa kibiashara ukilinganisha na miji mingine hapa nchini na ndio jiji linaloongoza kwa msongamano mkubwa wa magari.

Jiji hili la Dar es Salaam lina eneo la ukubwa wa kilomita za mraba zipatazo 1,800, kati ya hizo, kilomita za mraba 1,350 ni eneo la nchi kavu ikijumuisha visiwa nane vilivyopo katika eneo la Bahari ya Hindi.

Utafiti uliofanywa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) mwaka 2020 umebaini kuwa kwa upande wa Biashara, jiji hili kubwa, hupoteza asilimia 20 za faida zao kutokana na foleni za magari kwenye barabara za Dar es Salaam.

Kutokana na umuhimu wa jiji hili katika kuliingizia mapato Taifa, Serikali ya Mama Samia, imefanya jitihada za kupunguza foleni ikiwemo ujenzi wa daraja za juu (Flyovers) na ujenzi wa Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi (BRT) ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia.

Mbali na ujenzi huo, Serikali inafanya mazungumzo na kampuni ya China Overseas Engineering Group Co. Ltd. (COVEC) ambayo imeonesha nia ya kuwekeza Dola za Marekani Bilioni 1 (zaidi ya Shilingi Trilioni 2.7) kujenga barabara zenye lengo la kupunguza kero ya foleni jijini Dar es Salaam.

Kampuni hiyo ya China, COVEC inatarajiwa kujenga Barabara 10 za mzunguko (Ring roads) kupunguza foleni Jijini Dar es Salaam, ambapo Barabara hizo ni pamoja na barabara sita za ndani (Inner ring roads) na barabara nne za nje (Outer ring roads).

Kukamilika kwa ujenzi wa barabara hizo kunatarajiwa kupunguza foleni kwenye barabara kuu za Dar es Salaam, kwani magari yataweza kutumia barabara za kuzunguka zenye malipo (Toll roads).

Dar es Salaam ni moja ya Miji inayokuwa kwa kasi zaidi Barani Afrika na hivyo kukumbwa na kero kubwa ya foleni, hususan nyakati za asubuhi na jioni.

Kampuni hiyo ya COVEC inataka kutekeleza mradi huo wa kimkakati kwa njia ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha PPP, David Kafulila, amesema kuwa Mwekezaji huyo tayari amefanya kazi za awali, kama vile Upembuzi yakinifu na Uchambuzi wa Kiuchumi (Preliminary Feasibility Study).

Kampuni ya COVEC sasa inataka kuingia katika Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding-MOU) na Serikali ili iweze kufanya Upembuzi Yakinifu kamili (Full Feasibility Study) ya mradi huo.

Kampuni ya COVEC ya China ina uzoefu wa kujenga miradi ya miundombinu mikubwa na ya saizi ya kati kwenye takribani nchi 100 Duniani, yenye jumla ya thamani ya Dola za Marekani Bilioni 12.22.

Miradi iliyotelekezwa na kampuni hiyo inayomilikiwa na Serikali ya China ni pamoja na ujenzi wa barabara, nyumba, madaraja, miradi ya maji, umeme na sekta nyingine.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.