LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia amlilia Dkt. Ngugulile

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea kwa masikitiko kifo cha Mbunge wa Kigamboni ambae pia ni Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile kilichotokea usiku wa kuamkia Jumatano Novemba 27,2024.

Dkt. Ndugulile amefikwa na umauti akiwa kwenye matibabu nchini India.

Katika masikitiko yake, Rais Samia ameandika kwenye kurasa zake za kijamii kuwa;

Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, kilichotokea usiku wa kuamkia Jumatano Novemba 27, 2024.

Ninatoa salamu za pole kwa familia, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wananchi wa Kigamboni, ndugu, jamaa, marafiki na watanzania wote.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema, Amina" ameandika Rais Dkt. Samia.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.