Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi wa taasisi tatu
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wa taasisi tatu muhimu nchini baada ya baadhi ya viongozi waliokuwa wakioongoza taasisi hizo kumaliza muda wao.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi. Sharifa Nyanga, Rais Dkt. Samia amemteua Prof. David Homeli Mwakyusa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Amemteua IGP Mstaafu Said Ally Mwema kuwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania (TSN), ambaye anachukuwa nafasi ya Bw. Hab Mkwizu aliyemaliza muda wake.
Mhandisi Mussa Bally Natty ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB), akichukuwa nafasi ya Joseph Odo Haule ambaye amemaliza muda wake.
#KaziInaongea
No comments: