LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia aimarisha uchumi wa Tanzania duniani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Falsafa ya Diplomasia ya Uchumi chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeimarisha nafasi ya Tanzania duniani kupitia ushirikiano wa kibiashara, uwekezaji na maendeleo ya kiuchumi.

Rais Dkt Samia amekuwa mstari wa mbele kutumia mikutano ya kimataifa, ziara za kikazi na majadiliano na viongozi mbalimbali wa kimataifa ili kuvutia wawekezaji kutoka nje na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.

Kupitia juhudi hizo, Tanzania imepata ukuaji wa kasi katika sekta kama madini, utalii, kilimo na nishati, huku kukiwa na miradi mipya mingi inayoibuliwa.

Tanzania imepata sifa kubwa kimataifa kama nchi inayoongoza kwa kuvutia uwekezaji mkubwa katika sekta ya madini, hasa kutoka kwa makampuni ya madini ya Australia.

Kutokana na falsafa ya diplomasi ya uchumi, Rais Samia amefanikiwa kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara Afrika Mashariki na kimataifa kwa kuboresha miundombinu na diplomasia ya uchumi.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.