LIVE STREAM ADS

Header Ads

Utendaji wa Rais Samia wapunguza kasi ya vijana kukimbilia mjini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Maendeleo yanayopelekwa vijijini na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan yamesaidia kupunguza kasi ya vijana wengi kukimbilia mjini kutafuta maisha.

Kusambazwa kwa umeme, maji, barabara na huduma nyengine muhimu kwenye miji, vijiji na vitongoji, pamoja na kuwepo kwa mikopo isiyo na masharti inayotolewa na Rais Samia kumewahamasisha vijana kubaki huko waliko na kuanzisha biashara zinazowaingizia vipato.

Katika Mjadala wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao wako jijini Arusha kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 25 ya Jumuiya hiyo, Rais Samia amesema kwa Tanzania sasa wimbi la vijana kutoka vijijini kuja mjini limepungua.

Amesema hiyo imesababishwa na kupelekwa kwa maendeleo yanayopatikana mijini kule vijijini waliko.

"Wimbi la kuja mjini limepungua kwa sababu kule walipo wanapata yote ambayo mjini yanapatikana, kila kitu walichokuwa wakikifuata mjini sasa wanakipata kule waliko” amesema Rais Samia.

“Tanzania tumejitahidi kusambaza umeme katika Vijiji vyote japokuwa sio kila mtu ana umeme ila tunaendelea kuwasambazia wananchi na tunataka umeme ufike kote".

Akizungumzia masuala ya mabadiliko ya tabianchi amesema yana gharimu nchi na akatolea mfano Tanzania inatumia asilimia 4 mpaka 5 ya pato la Taifa kwenye masuala ya kupambana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema moja ya njia ya kukabiliana na hali hiyo ni kuepukana na matumizi ya kuni na mkaa, badala yake serikali inahakikisha Nishati ya gesi inafika katika maeneo mengi ya nchi na lengo ni kuwaondoa akina mama kwenye matumizi ya kuni na mkaa.
#KAZIINAONGEA 

No comments:

Powered by Blogger.