Benki ya CRDB yatoa mafunzo kwa Mawakala wake Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Benki ya CRDB imeendelea kutoa elimu, mafunzo na kuwajengea uwezo mawakala wake katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma za kifedha ili kuzidi kutoa huduma bora kwa wateja.
Akizungumza kwenye mafunzo yaliyofanyika Jumamosi Novemba 30, 2024 jijini Mwanza, Meneja wa CRDB tawi la Rock City, Jesca Kikoito aliwataka mawakala wa benki hiyo kuendelea kuwa mabalozi wazuri kwa kutoa huduma bora.
Mafunzo yanayotolewa na benki ya CRDB kwa mawakala wake nchini ni pamoja na namna utoaji huduma bora kwa wateja, huduma za kibenki, udhibiti wa utakatishaji fedha na elimu ya ujasiriamali.
Mbali na mafunzo hayo, pia benki ya CRDB imewatambua mawakala bora wa mwaka mkoani Mwanza ambao wamekuwa wakitoa huduma bora kwa wateja, wamekuwa mabalozi wazuri wa benki hiyo na ambao biashara zao zimekuwa kwa mwaka 2024.
Meneja wa CRDB tawi la Rock City, Jesca Kikoito akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa mawakala wa CRDB mkoani Mwanza.
Meneja wa CRDB tawi la Rock City, Jesca Kikoito akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mawakala mkoani Mwanza walioshiriki mafunzo wakimsikiliza Meneja wa CRDB tawi la Rock City, Jesca Kikoito.
Meneja Mauzo CRDB Makao Makuu, Goodluck Ruhaga akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Meneja Mauzo CRDB Makao Makuu, Goodluck Ruhaga akizungumza wakati wa mafunzo kwa mawakala wa benki hiyo mkoani Mwanza.
Meneja Uhusiano CRDB Kanda ya Ziwa, Erasto Alfred akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Mmoja wa mawakala wa CRDB Mwanza akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mmoja wa mawakala wa CRDB Mwanza akichangia mada.
Meneja wa CRDB tawi la Rock City, Jesca Kikoito (katikati) akikabidhi cheti kwa mmoja wa mawakala wa benki hiyo waliofanya vizuri kwa mwaka 2024.
Meneja wa CRDB tawi la Rock City, Jesca Kikoito (wa pili kulia) akikabidhi cheti kwa mmoja wa mawakala wa benki hiyo waliofanya vizuri kwa mwaka 2024.
Wasimamizi wa mawakala wa CRDB Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mawakala 10 bora waliofanya kazi vizuri mwaka 2024 wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa benki hiyo akiwemo Meneja wa CRDB tawi la Rock City, Jesca Kikoito.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: