Filamu ya The Royal Tour yazidi kuvuta watalii Tanzania
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Filamu hii iliyoonekana kuvutia katika Sekta ya Utalii nchini, imewavutia wageni kuja kuwekeza katika Madini, na Taifa linajivunia uwekezaji katika sekta hiyo kwa kuwa Tanzania tuna madini ya kutosha.
Kufuatia filamu ya Royal Tour kuwavutia wengi, watu Bilioni 1.2 wamehusika moja kwa moja kuona, kutazama, kuangalia na kuifuatilia Tanzania kutokana na filamu ya Royal Tour iliyotangazwa na Rais Dkt. Samia, huku Hifadhi za Taifa zikivunja rekodi kwa kupata jumla ya watalii 1,412,719 kwa kipindi cha miezi tisa, idadi ambayo haijawahi kuipata.
Aidha, kumekuwa na ongezeko la mapato ya Utalii maradufu ambapo mapato ya jumla ya sekta yameongezeka kutoka Dola za Marekani Shilingi Bilioni 1.310.34 (sawa na Shilingi Trilioni 3.01) mwaka 2021 hadi Dola za Marekani Shilingi Bilioni 2.527.77 (sawa la Shilingi Bilioni 5.82).
Ni ukweli usiopingika kuwa, Tanzania imejaliwa kuwa na madini aina nyingi na kuwepo kwa madini kumesaidia ongezeko la wazalishaji, wadogo, wa kati na wakubwa, hivyo kabla ya mwekezaji kufanya shughuli za uchimbaji ni lazima afuate masharti ya uwekezaji ikiwa ni kwa kuandaa taarifa ya athari za mazingira wakati wa uchimbaji madini na namna ya kurejesha katika hali yake ya asili baada ya uchimbaji, ambapo Madini kama Uranium tathmini yake inafanyika kwa mapana zaidi.
Katika kusimamia Uwekezaji na shughuli za uchimbaji wa madini, Wizara ya Madini ina vitengo vyote vinavyosimamia masuala ya afya, usalama na utunzaji mazingira kikiwemo cha ukaguzi wa migodi.
Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Madini, kwa kununua mitambo mikubwa, mitano ambayo ilishawasili nchini, kumi ipo njiani inakuja.
Rais Dkt. Samia ameagiza mitambo kuletwa kwa mitambo hiyo itakayowarahisishia wachimbaji wadogo kupata taarifa za uchimbaji na kuwaepusha na hasara.
Rais ameagiza mitambo hii ikifika igawanywe kote ambapo miongoni mwa mitambo hiyo, itengwe miwili kwa ajili ya vijana na mmoja kwa ajili ya wanawake.
Mpango wa Serikali ni kuhakikisha kuwa sekta hii inachangia asilimia 10 au zaidi katika Pato la Taifa ifikapo 2025 na ukuaji wa Sekta ya Madini umeongezeka kutoka asilimia 9.4 Mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 11.3 mwaka 2023.
Kutokana na kuendelea kuimarika kwa Sekta, Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa utaongezeka na kufikia asilimia 10 au zaidi ifikapo Mwaka 2025 kama ilivyoelezwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.
Serikali kupitia Tume ya Madini inarudisha minada ya ndani ya madini ya vito itakayofanyika katika maeneo ya uzalishaji hususan Mirerani, Mahenge, Tunduru, Dar es Salaam, Arusha na Tanga na Kimataifa itafanyika Mji wa Bangkok na Jaipur nchini India.
Uendeshaji wa minada hiyo ni fursa muhimu ya kutangaza madini ya vito yanayozalishwa hususan kwenye Masoko ya Kimataifa ambayo ni njia mojawapo ya kuwafikisha Watanzania katika masoko ya uhakika na upatikanaji wa bei nzuri na stahiki.
#KaziInaongea
No comments: