LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mtandao wa wanawake watetezi wa haki za binadamu (CWHRD) waadhimisha Siku 16 za Kupinga Ukatili

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Jitihada za utoaji elimu katika jamii zinazofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, zimetajwa kusaidia kupunguza matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi.

Hayo yalielezwa Disemba 03, 2024 na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Davis Ulotu wakati akizungumza kwenye mdahalo wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Igogwe iliyopo Kata ya Shibula.

Mdahalo huo uliandaliwa na mashirika ya zaidi ya 10 yanayounda mtandao wa wanawake watetezi wa haki za binadamu Tanzania (CWHRD), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yaliyoanza Novemba 25 na kufikia tamati Disemba 10, 2024.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Igogwe walieleza kunufaika na mdahalo huo kwa kupata uelewa utakaowasaidia kujiepusha na vishawishi mbalimbali vinavyoweza kusababisha wakatishe ndoto yao ya masomo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Davis Ulotu akizungumza kwenye mdahalo huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la SAWAU, Sophia Donald akizungumza kwenye mdahalo huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Teens Corridor, Sophia Nshushi akizugumza kwenye mdahalo huo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.