LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia kuwa mwenyeji wa Marais wa Afrika

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com 
Siku 30 zimesalia kuelekea mkutano mkubwa wa nishati wa wakuu wa nchi za Afrika uliobeba ajenda ya upatikanaji wa haraka wa nishati barani Afrika.

Mkutano huo muhimu kwa mustakabali wa mazingira ya Afrika unatarajiwa kufanyika Dar es Salaam, Tanzania na utahudhuriwa na marais wa nchi mbalimbali za Afrika wakiongozwa na mwenyeji wao Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae amebeba agenda ya nishati safi ya kupikia Afrika.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Januari 27 & 28, 2025 katika kituo cha mikutano Mwalimu Nyerere (JNICC ).

 Hii ni fursa kubwa kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo, hususani katika upande wa kiuchumi kwa wafanyabiashara wanaotoa huduma mbalimbali za kijamii. KAZI INAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.