LIVE STREAM ADS

Header Ads

Chuo cha michezo Malya Mwanza chaboreshwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com 
Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwekeza katika Sekta ya Michezo, kwa kuboresha miundombinu ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya, kilichopo Kwimba mkoani Mwanza, ambapo kinatarajia kusajili wanafunzi zaidi ya 500 kwa mwaka 2025.

Kuboreshwa kwa miundombinu ya chuo hicho, ni kutokana na jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuinua michezo nchini.

Aidha Mkuu wa Chuo hicho, Dkt.John Tiboroha hivi karibuni amesema kuwa, Chuo hicho, kinatoa taaluma ya Michezo (Physical Education), kwa kuwafundisha walimu, wanaoenda kufundisha michezo mashuleni.

"Matarajio yangu kwa chuo hiki ni makubwa, kwa sababu tunajenga mabweni yatakayo chukuwa wanafunzi zaidi ya 500, na kuna mabweni mengine yanajengwa huko yatakuwa yanachukuwa zaidi ya wanafunzi 300" amesema.

Amesema mabweni mengine yanatarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni, na hivyo kuanzia mwakani wataanza kuchukuwa wanafunzi wengi kwa kuwa nafasi ni nyingi na Serikali imeongeza bajeti kwenye Wizara ya Michezo, ili miundombinu kama hii iweze kuwanufaisha Watanzania kwenye michezo siku za usoni.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeendelea kuwekeza nguvu nyingi, pamoja na miradi ya kimkakati ili kuwavutia Watanzania wasome na kupata fursa za kimichezo Ulimwenguni. KAZI INAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.