LIVE STREAM ADS

Header Ads

Milioni 220 kuboresha miundombinu ya utalii Tabora Zoo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika jitihada za kuinua Sekta ya Utalii nchini, imetoa zaidi ya Shilingi Millioni 220, kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa ajili ya maboresho ya miundombinu ya Utalii ndani ya bustani ya Wanyamapori hai "Tabora ZOO"

Rais Dkt. Samia, amekuwa mstari wa mbele katika kuinua Sekta ya Utalii na Uwekezaji, katika kipindi cha uongozi wake wa miaka mitatu.

Fedha hizo zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zimetolewa kwa lengo la kuboresha Miundombinu ndani ya bustani hiyo.

Afisa Wanyamapori Mkuu kutoka Kanda ya Magharibi ya TAWA, Jovin Nachihangu amesema, Jengo hilo la Kitalii ndani ya bustani hiyo, litatumiwa na wananchi kupata taarifa za vivutio vya utalii vinavyopatikana katika bustani hiyo na Kanda ya Magharibi kwa ujumla (Visitors Information Centre - VIC).

Katika jengo hilo pia kutakuwa na vyoo vya kisasa kwa ajili ya wageni na mabanda ya Wanyamapori walao nyama (Simba, Chui, Duma).

“Kabla ya maboresho ya miundombinu ya Utalii, TAWA tulikuwa tunakusanya Shilingi Milioni moja kwa mwaka, lakini baada ya maboresho katika kipindi hiki cha miaka 3 TAWA inakusanya kupitia bustani hii kiasi kisichopungua Shilingi Millioni 50 kwa Mwaka na bado tunaendelea kuhakikisha kwamba mapato yanaendelea kuongezeka” amesema Jovin.
#KAZIINAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.