LIVE STREAM ADS

Header Ads

Benki ya Dunia yaunga mkono jitihada za Rais Samia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipambanua katika kuleta usawa wa kijinsia.

Ili kulifanikisha hilo Serikali na Benki ya Dunia (WB) hivi karibuni wamesaini mikataba miwili yenye thamani ya dola za Marekani milioni 104,ambazo ni sawa na takriban shilingi bilioni 248.

Fedha hizo zitatukika katika kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Nchini Tanzania maarufu kama “PAMOJA”.

Mchanganuo wa mikataba hiyo uko kama ifuatavyo, mkataba wa dola za Marekani milioni 4, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 9.5 ni msaada na mkataba wa dola za Marekani milioni 100, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 238 ni mkopo wenye masharti nafuu.

Mradi wa PAMOJA uliosainiwa utasaidia kuongeza upatikanaji wa fursa za kiuchumi kwa Wanawake pamoja na huduma za kuzuia na kukabiliana na ukatili wa kijinsia Tanzania Bara na Zanzibar ambapo mradi utatimizwa kupitia uimarishaji vikundi vya wanawake kwa kuwajengea ujuzi wa biashara na kuwaunganisha na fursa za masoko, kuongeza fursa za mikopo nafuu kwa vikundi vya wanawake, kuwaongezea upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia mifumo rasmi ya kifedha pamoja na kuimarisha huduma za kukabiliana na ukatili wa kijinsia.

Aidha mradi huo utawanufaisha moja kwa moja Wanawake wapatao 319,850 na walengwa wengine 399,000, wakiwemo wanafamilia za wanufaika.
#KAZIINAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.