LIVE STREAM ADS

Header Ads

Usiku wa Wanahabari na Wadau wa Habari 2024 wafanya Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waandishi wa Habari mkoani Mwanza wamekumbushwa kuzingatia maadili ya taaluma yao wakati wanatimiza majukumu ya kila siku ili jamii ijengwe kwenye misingi ya ukweli.

Rai hiyo imetolewa Disemba 13, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Christopher Ngubiagai kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye hafla ya usiku wa wanahabari na wadau wa haari ulioandaliwa na klabu ya wanahari Mwanza (MPC).

Amebainisha vyombo vya habari ni muhimili muhimu hivyo ili kuepuka migongano isiyo na tija waandishi wa habari wana wajibu wa kujiridhisha na usahihi wa kile wanachokusudia kuwafahamisha wananchi.

"Ndugu zangu wana habari wote hapa ni mashuhuda Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan anavyozidi kuwawekea mazingira mazuri ya kazi zenu na hasa anavyosisitiza ushirikiano baina ya Serikali na vyombo vya habari, tuendelee kutumia kalamu zetu vizuri na hata pale kwenye kukosoa uungwana utumike na isiwe karaha kwa mlengwa" amesema.

Ngubiagai amesema Mwanza kuna miradi mingi ya kimkakati, waandishi wa habari wanatakiwa kuimulika ili wananchi wapate ufahamu wa kina namna Serikali yao inavyowaletea maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa MPC, Edwin Nsoko amesema ni utaratibu waliojiwekea wa kila mwaka kuwa na usiku wa pamoja kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na kubadilishana uzoefu wa shughuli zao.

"Kazi zetu zinahitaji ushirikiano wa dhati ili kutimiza vizuri majukumu yetu, hapa zipo Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi ambazo tumeshirikiano nazo kuhakikisha tunajenga uchumi wa Taifa letu" amesema.

"Hivi sasa tunazidi kujiimarisha katika sekta ya usafiri wa maji kwenye maziwa ya Victoria,Tanganyika na Nyasa. Meli mpya ya MV. Mwanza iko mbioni kuanza safari zake na itafika hadi Kenya na Uganda. Ni dhahiri shughuli za kiuchumi zitapiga hatua hivyo vyombo vya habari vina wajibu wa kuwaemisha wananchi" amesema Erick Hamisi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji TASHICO.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.