LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri wa Afya mgeni rasmi kongamano la wenye ulemavu Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Jukwaa la wadau na mashirika yanayowasaidia watu wenye ulemavu la PAMOJA CONSORTIUM limeandaa kongamano kwa ajili ya kutafuta njia bora ya kutatua changamoto zinazokabili kundi hilo katika jamii. 

Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Bishop Mayala Nyakahoja jijini Mwanza kuanzia tarehe 16-17 Januari 2025 huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Afya, Jenista Mhagama. 

Katika kongamano hilo, mdau mwenyeji ni kituo cha kulea watoto wenye ulemavu cha Huruma kilichopo Pasiansi wilayani Ilemela. Wadau hao wamekutana na wanahabari jijini Mwanza, Januari 16, 2025 na kutoa mwelekeo wa kongamano hilo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.