Mjasiriamali wa mikate Mwanza afungua Kituo cha Mafuta (Fulano Petrol Oil)
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mjasiriamali wa mandazi na mikate jijini Mwanza, Stephano Fulano ameingia kwenye orodha ya waliothubutu na kuweza baada ya kufanikiwa kufungua kituo cha mafuta katika eneo la Usagara.
Akizungumza Jumanne Februari 28, 2025 wakati wa ufunguzi wa Kituo hicho, Fulano amesema sera nzuri za uwekezaji za Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zimemsaidia kutimiza ndoto hiyo kubwa na kwamba mkakati uliopo ni kufungua matawi zaidi nchini.
“Kupitia kampuni ya Fulano General Suppy inayoshughulika na uzalishaji wa mandazi, mikate, biskuti na usafirishaji wa mizigo, tumefanikiwa kufungua kituo cha mafuta Fulano Petrol Oil na hivyo kutimiza ndoto yangu ya muda mrefu” alisema Fulano.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Emmanuel Masangwa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kituo hicho alisema lengo la Serikali inayoongozwa na chama hicho ni kuweka mazingira bora ya kuwakuza wafanyabiashara ili kuendelea kutoa fursa ikiwemo za ajira kwa watanzania.
Awali akizungumza kwenye misa ya ufunguzi wa Fulano Petrol Oil, Pardi Vincent Shigi kutoka Parokia ya Ilemela alisema uwekezaji huo unaendana na maandiko matakatifu yanayosisitiza watu kuwa wabunifu na kufanya kazi halali ili kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao.
Kituo cha mafuta Fulano Petrol Oil kinapatikana Kata ya Usagara wilayani Misungwi kilipokuwa awali kituo cha mafuta Smart Usagara baada ya kufanyika mabadiliko ya kiuwekezaji.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa Kituo cha Mafuta Fulano Petrol Oil, Stephano Lucas Fulano akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kituo hicho kilichopo Usagara wilayani Misungwi.
Mkurugenzi wa Kituo cha Mafuta Fulano Petrol Oil, Stephano Lucas Fulano akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kituo hicho kilichopo Usagara wilayani Misungwi.
Viongozi wa dini akiwemo Pardi Vicent Shigi kutoka Parokia ya Ilemela wakiongoza misa takatifu kabla ya ufunguzi rasmi wa kituo cha mafuta Fulano Petrol Oil kilichopo Usagara Misungwi mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Emmanuel Masangwa (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha mafuta cha Fulano Petrol Oil. Kushoto ni Mkurugenzi wa kituo hicho, Stephano Lucas Fulano.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria ufunguzi huo.
Wananchi wakiwa kwenye ufunguzi huo.
Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa kwenye ufunguzi wa kituo cha mafuta Fulano Petrol Oil.
Fulano Petrol Oil, Usagara wilayani Misungwi.
Smart Usagara sasa ni Fulano Petrol Oil.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: