LIVE STREAM ADS

Header Ads

Gugumaji jipya tishio Ziwa Victoria, NECM yachukua hatua

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shughuli za uwekezaji zisiyofuata uhifadhi endelevu na tathmini ya athari za mazingira katika Ziwa Victoria, zimetajwa kasababisha Gugumaji jipya aina ya Salvinia kuibuka katika Ziwa hilo na kuhatarisha maisha ya viumbe hai ikiwemo samaki na huduma za usafiri wa vivuko (feri) katika maeneo ya Kamanga na Busisi mkoani Mwanza. 

Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Baraza (NEMC) Kanda ya Ziwa, Jarome Kayombo ameyasema hayo Jumapili Machi 02,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza kuhusu utafiti uliofanywa na kikosi kazi kilichoundwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza baada ya kuibuka kwa Gugumaji hilo mwanzoni mwa mwezi Januari 2025.

Kayombo alibainisha kuwa utafiti wa awali umebaini uwepo wa virutubisho vinavyoweza kasababisha mimea kuota katika Ziwa Victoria ikiwa ni ishara ya uchafuzi wa Ziwa hilo kutokana na shughuli za binadamu kama kilimo na ufugaji.

Alisema NEMC imeandaa mpango kazi wa kufanya ukaguzi na utoaji elimu kwa wawekezaji wakiwemo wafugaji wa samaki kwa njia ya vizimba katika Ziwa Victoria ili kuhakikisha shughuli zao zinafanyika kwa kuzingatia uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

Naye Meneja Mawasiliano NEMC, Irene John alisema kila mwananchi anao wajibu wa kuhakikisha anajiepusha na uchafuzi wa Ziwa Victoria kwa matumizi ya vizazi vya sasa na baadae.

"Wawekezaji tunawahitaji lakini tunataka uwekezaji ambao ni endelevu, isije kufikia hatua vizazi vijavyo vinasimuliwa hapa tulikuwa na Ziwa Victoria lakini Gugumaji lilitanda kwa sababu hatukujali mazingira. Hatujachelewa, mimi na wewe tunaweza kusaidia kunusuru uzuri wa Ziwa hili" alisema John.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Baraza (NEMC) Kanda ya Ziwa, Jarome Kayombo akizungumza na wanahabari jijini Mwanza.
Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Baraza (NEMC) Kanda ya Ziwa, Jarome Kayombo (kushoto) akizungumza na wanahabari jijini Mwanza. Kulia ni Meneja Mawasiliano NECM, Irene John.
Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Baraza (NEMC) Kanda ya Ziwa, Jarome Kayombo akizungumza na wanahabari jijini Mwanza.
Maafisa mbalimbali wa NEMC.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.