Majaliwa aonya tabia za kigeni, zisizo za maadili
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Hayo yamesemwa Machi 19, 2025 katika Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Msaidizi Mstaafu wa Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki Bukoba Askofu Method Kilaini.
“Sote tumekua tukishuhudia ongezeko la vitendo vya ukosefu wa maadili katika jamii. Vitendo hivi vinatokana na malezi hafifu lakini pia watu kuiga mila na desturi kutoka mataifa mengine ambazo haziendani na tamaduni na maadili yetu ya Kitanzania” alisema Majaliwa.
Majaliwa alisema hali hiyo imeathiri mwenendo wa jamii, hususan kwa vijana ambapo wanashuhudia mabadiliko katika misingi ya familia, jamii, na Taifa kwa ujumla. “Nitumie fursa hii kuliomba Kanisa kuendelea kuwa nguzo ya maadili bora, kwa kutoa mwongozo wa kiroho na kijamii”.
Alisema Kanisa lina nafasi ya pekee katika kuhakikisha Taifa linarudisha maadili ya kweli ya Kitanzania yanayofundisha kuheshimu utu, haki, na amani. “Serikali, tunatambua mchango mkubwa wa Kanisa katika hili na tutashirikiana nalo ili kuleta mabadiliko chanya kwa kizazi cha sasa na kijacho”.
Alisema kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wa madhebu ya dini ikiwemo Kanisa Katoliki katika kuboresha ustawi wa jamii yetu, hivyo amewaomba viongozi wa dini nchini waendelee kuwa nguzo ya maadili bora, kwa kutoa mwongozo wa kiroho na kijamii.
Akizungumza kuhusu Askofu Kilaini, Majaliwa alisema ni kielelezo cha ujasiri, imani thabiti, na huduma ya kujitolea kwa Kanisa na jamii ya Watanzania, ameonesha nguvu ya uvumilivu, akiwa na michango mikubwa katika maisha ya kanisa.
KAZI INAONGEA
No comments: