LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kampeni ya Furaha ya Binti yawafikia wanafunzi Misungwi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Afya Radio 96.9 Mwanza kupitia kampeni yake ya Furaha ya Binti imetoa elimu ya hedhi salama pamoja na mahitaji mbalimbali ikiwemo taulo za kike kwa wanafunzi wa shule msingi Mitindo iliyopo wilayani Misungwi.

Hatua hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani yaliyofanyika Alhamisi Mei 28, 2025 ikiwa ni mwaka wa pili mfululizo kampeni ya Furaha ya Binti kufanyika ambapo kwa mwaka jana iliwafikia wanafunzi wa shule ya sekondari Buzuruga wilayani Ilemela.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mratibu wa kampeni ya Furaha ya Biti, Esther Baraka ambaye pia ni Mkuu wa Vipindi Afya Radio, alisema lengo la kampeni hiyo ni kurejesha shukurani kwa jamii kwa kuwasaidia wenye uhitaji huku wakitoa elimu ya hedhi salama kama ilivyo lengo la kuimarisha uelewa kwa jamii kuhusu masuala ya afya.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mitingi akiwemo Leticia Jackson na Mariam Paschal walioa shukurani kwa Afya Radio kupitia kampeni ya Furaha ya Binti kwa mahitaji waliyotoa, kuwaelimisha kuhusu hedhi salama na kwamba watafikisha elimu hiyo kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuvaa pedi mfululizo kwa muda usiozidi masaa matatu.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.