LIVE STREAM ADS

Header Ads

Madini ya zaidi ya Tsh. Bilioni moja yakamatwa jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza vimekamata madini ya almasi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.715 katika uwanja wa ndege wa Mwanza yaliyokuwa yakisafirishwa bila vibali kwenda nje ya nchi na raia mmoja wa kigeni.

Hayo yamebainishwa Ijumaa Mei 23, 2024 majira ya saa nne usiku na Waziri wa Madini, Antony Mavunde wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza.

Mavunde ameonya kuwa Serikali imeboresha mazingira ya biashara ya madini nchini kwa kuondoa utitiri wa kodi na kuanzisha masoko na vituo vya kuuzia madini hivyo hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kwenda kinyume na sheria na taratibu za biashara hiyo.

Hili ni tukio kubwa la pili la madini kukamatwa jijini Mwanza ambapo itakumbukwa Januari 04, 2019 shehena ya madini ya dhahabu yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 30 ilikamatwa ikisafirishwa kwa gari wilayani Sengerema ambapo madini hayo yalitaifishwa na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.