Wizara ya Maendeleo ya Jamii Yashiriki Mei Mosi Singida
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

📌 Machinga wamshukuru Rais Samia kwa mikopo yenye masharti nafuu.
📌 Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yapaza sauti mazingira mazuri utendaji kazi wao.
📌 Wanawake wamshukuru Rais Samia kwa Majukwaa Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi.
📌 Wadau wa Vituo vya kuleta Watoto waahidi katika Malezi Bora kwa Watoto.
Na WMJJWM- Singida
Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, imeshiriki maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani, iliyofanyika Mei 1, 2025, Mkoani Singida.
Katika maadhimisho hayo Makundi mbalimbali yanayoratibiwa na Wizara yameshiriki huku yakimpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuweka mazingira bora katika Ustawi wa Makundi hayo.
Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) ambao walibeba bango lenye ujumbe wa kumshukuru Rais Samia kwa fursa ya mikopo yenye masharti nafuu inayosaidia kukuza biashara zao na kuongeza kipato.
Mmoja wa mfanyabishara ndogondogo Samwel Mihiko amesema fursa hiyo inadhihirisha juhudi za Rais kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum,ambayo ndiyo yenye dhamana kusimamia wafanyabiashara hao.
Kwa upande wa Majukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi mmoja wa mjumbe wa Majukwaa hayo Mkoa wa Singida Anitha James amemshukuru Rais Samia kwa fursa za mikopo kwa Wanawake inayowawezesha kuongeza mitaji na kujikwamua kiuchumi.
"Sisi tunamshukuru sana Rais Samia hakika ameendelea kutuona sisi Wanawake katika shughuli tunazofanya na kupitia Majukwaa haya ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi tumeweza kupata fursa nyingi sana za kiuchumi" amesema Anitha
Naye mmoja ya mdau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Neema Silvester amesema kuwa mazingira mazuri ya utendaji kazi wa Mashirika hayo katika mikoa na Halmashauri mbalimbali yamesaidia Mashirika hayo kutekeleza miradi mbalimbali inayounga jitihada za Serikali katika kuleta maendeleo nchini.
Akizungumza mara baada ya Maadhimisho hayo mdau kutoka Vituo vya Malezi kwa Watoto mchana mkoani Singida Alfred Mbogela amesema kwa mazingira mazuri yaliyowekwa na Serikali ya Rais Samia kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii Vituo hivyo vitaendelea kutoa huduma bora hasa kwa kutoa malezi bora na kuimarisha ulinzi kwa watoto hao.
Kwa mwaka huu Maadhimisho Siku ya Wafanyakazi Duniani yameongozwa na Kaulimbiu isemayo: ”Uchaguzi Mkuu 2025 Utuletee Viongozi Wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki.
No comments: