King Oil Achukua Fomu Kuwania Ubunge Itwangi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Suleiman Nassor Said 'King Oil'

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga na mfanyabiashara wa mafuta, Suleiman Nassor Said maarufu kama King Oil, leo Juni 30, 2025, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo Jipya la Itwangi.
Jimbo la Itwangi ni jimbo jipya lililokatwa kutoka Jimbo la Solwa, mkoani Shinyanga.
Suleiman Nassor Said ambaye ni mzaliwa wa Tinde, amesema ameamua kuchukua fomu hiyo ili kuendeleza juhudi zake za kuwaletea wananchi maendeleo, akitumia uzoefu wake wa kuwasogezea huduma mbalimbali za kijamii.
No comments: