LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kogogo CRDB achukua fomu Jimbo la Kisesa wilayani Meatu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Meneja Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta (kushoto) amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kisesa lililopo Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.

Hatua hiyo inaongeza joto la uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo hilo ambalo kwa sasa mbunge wake ni Luhaga Mpina.
Sitta ameweka wazi maono na ahadi zake kwa wana Kisesa ikiwa atapata ridhaa ya kuwa mbunge wao kuwa ni pamoja na;

Kutahakikisha Kisesa inapata maji safi kupitia visima na miradi ya maji ya kudumu.

Pia kupigania bajeti ya kujenga au kuboresha shule na zahanati vijijini.

"Nitahamasisha vijana kujiunga na vikundi vya uzalishaji na nitawatafutia mitaji na mafunzo" amesisitiza Sitta.

Ameongeza kuwa atafanya kazi vyema na Serikali ili kuhakikisha barabara kuu na za vijijini zinajengwa au kukarabatiwa ili zipitika wakati wote.

No comments:

Powered by Blogger.