LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mtandao wa GRBA Wapitia Bajeti 2025/26 kwa Jicho la Kijinsia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Wadau wa Mtandao wa Bajeti yenye Mrengo wa Kijinsia (Gender Responsive Budgeting Alliance - GRBA) unaoratibiwa na Mtandao wa Kijinsia TGNP, wamekutana leo Ijumaa, Juni 13, 2025, katika ukumbi wa TGNP Jijini Dar es Salaam, kufuatia kuwasilishwa kwa Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/26 na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).

Warsha hiyo imelenga kutathmini Bajeti ya Taifa kwa jicho la kijinsia, pamoja na kujadili mafanikio, changamoto na mafunzo ya utekelezaji wa kazi za GRBA kwa mwaka uliopita. 

Aidha, wadau wamepitia Ripoti ya Beijing +30, kuchakata maeneo muhimu ya ufuatiliaji katika upangaji wa rasilimali, na kujadili mchakato wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O&OD) kwa ajili ya kuainisha maeneo ya kipaumbele ya utekelezaji katika ngazi ya jamii na taifa.

Tazama Matukio katika picha - Picha na Kadama Malunde
Wadau wa Mtandao wa Bajeti yenye Mrengo wa Kijinsia (Gender Responsive Budgeting Alliance - GRBA) unaoratibiwa na Mtandao wa Kijinsia TGNP wakiwa kwenye warsha leo Ijumaa, Juni 13, 2025, katika ukumbi wa TGNP Jijini Dar es Salaam wakitathmini Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/26.

No comments:

Powered by Blogger.