Mashindano ya Uhifadhi Simiyu yafika hatua ya fainali
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mashindano ya nyimbo za asili ya 'Dance for Conservation 2025' yanayoshirikisha vikundi vya akina mama katika Kata ya Lamadi wilaya ya Busega mkoani Simiyu, yamefikia hatua ya fainali huku yakivuta hisia za mashabiki wa nyimbo hizo.
Mashindano hayo yameandaliwa na taasisi ya uhifadhi wa wanyamapori ya Peace For Conservation, kwa lengo la kufikisha elimu ya uhifadhi hasa kujiepusha na ujangiri wa wanyamapori kama tembo katika jamii zinayozunguka hifadhi ya Taifa Serengeti na Pori la Akiba Kijereshi.
Katika Kijiji cha Lukungu, kikundi cha Wajasiriamali kimefanikiwa kutinga fainali baada ya kuchuana vikali na kikundi cha Mshikamano Ijumaa Julai 18, 2025 katika uwanja wa TAWA Kijereshi.
Katika Kijiji cha Kijilishi Jumamosi Julai 19, 2025, kikundi cha Amani kimefanikiwa pia kutinga fainali baada ya kuibuka kidedea mbele ya kikundi cha Ushirikiano, hivyo fainali itakuwa ya ushindani mkubwa baina ya Wajasiriamali kutoka Kijiji cha Lukungu na Amani kutoka Kijiji cha Kijilishi.
Mashindano haya yamefadhiliwa na shirika la Humane World for Animal ambapo mshindi wa kwanza ataibuka na kitita cha shilingi milioni moja huku mshindi wa pili akijinyakulia shilingi laki tano.
Fainali itafanyika Jumatatu Julai 20, 2025 katika uwanja wa Kijiji cha Kijilishi Lamadi wilayani Busega.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: