LIVE STREAM ADS

Header Ads

Dkt. Jingu ahimiza wahitimu Misungwi CDTTI kutumia ujuzi wao kwa maendeleo ya Taifa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum- Dkt. John Jingu amewahimiza wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi (Misungwi CDTTI), kutumia kwa weledi ujuzi wanaoupata chuoni hapo kwa maendeleo yao na taifa.

Dkt. Jingu ameyasema hayo Julai 04, 2025 wakati akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea na kukagua shughuli na taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika Mkoa wa Mwanza.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Arch. Charles Achuodho alitoaa shukurani kwa Serikali kwa kutoa fedha shilingi milioni 300 kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa hosteli ya ghorofa nne zilizotumika kukamilisha ujenzi wa msingi ambapo hadi kukamilika ujenzi huo utagharimu shilingi bilioni 2.2 likiwa na uwezo wa kubeba wanafunzi zaidi ya 700.

Awali Dkt. Jingu alitoa fursa kwa wanafunzi wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi kuzungumza ambapo waliomba Serikali kukamilisha ujenzi wa hosteli, ujenzi wa uzio, kukarabati majengo chakavu na kuongeza vifaa vya kujifunzia ili kuondokana na changamoto ziliopo.

Akiwa mkoani Mwanza, Dkt. Jingu pia alitembelea na kukagua shughuli za Kituo cha Wazee Bukumbi na Dawati la Huduma za Ustawi wa Jamii katika Stendi Kuu ya Mabasi Nyegezi na kutoa rai kwa jamii na wadau kushirikiana ili kutokomeza vitendo vya ukatili kwa makundi maalum ikiwemo watoto na wazee.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Misungwi CDTTI kilichopo mkoani Mwanza.
Wanafunzi wa Misungwi CDTTI wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu.
Wanafunzi wa Misungwi CDTTI wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu.
Mkuu wa Chuo cha Misungwi CDTTI, Arch Charles Achuodho akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu kuzungumza na wanafunzi. 
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Mwanza, Janeth Shishila akitoa salamu.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Mwanza, Janeth Shishila akitoa salamu.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu akikagua karakana ya uzalishaji tofali katika Chuo cha Misungwi CDTTI.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu akikagua maabara ya udongo katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi CDTTI.
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu, Mkuu wa Chuo cha Misungwi CDTTI Arch Charles Achuodho na Makamu Mkuu wa Chuo cha Misungwi CDTTI upande wa Taaluma- Dongo Nzori.
Wanafunzi wa Chuo cha Misungwi CDTTI.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Misungwi CDTTI.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Misungwi CDTTI.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Misungwi CDTTI.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu kwenye picha ya pamoja na watumishi na wanafunzi wa Misungwi CDTTI.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu kwenye picha ya pamoja na watumishi na wanafunzi wa Misungwi CDTTI.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.