Mwenyekiti wa INEC atembelea Gereza la Butimba kukagua zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com







Na Mwandishi Wetu, Mwanza.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Julai 03, 2025 amemtembelea na kukagua mwenendo wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Gereza Kuu la Butimba lililopo mkoani Mwanza na kushuhudia namna zoezi linavyokwenda kwa ufanisi.
Mzunguko wa tatu wa awamu ya pili ya uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Wafungwa chini ya miezi sita na mahabusu waliopo katika Magereza kwa Tanzania Bara na Vyuo vya Mafunzo Zanzibar ulianza Juni 28 na unataraji kukamilika Julai 04, 2025.







No comments: