LIVE STREAM ADS

Header Ads

Tanzania Yaimarisha Sekta ya Habari Kupitia Ushirikiano na Wadau – Prof. Kabudi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba akionyesha Kitambulisho cha Uandishi wa Habari (Press Card) kinachotolewa na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari-JAB mbele ya mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Phillip Mpango wakati wa ufunguzi rasmi Mkutano wa Pili wa Mtandao wa Mabaraza Huru ya Habari Afrika (NIMCA), uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC, Arusha.

Prof. Palamagamba Kabudi amesema Tanzania imeendelea kushirikiana na wadau wa habari pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya habari nchini. 

Amesema kupitia bajeti ya Serikali ya Mwaka 2025/2026, Serikali imeridhia kutoa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani kwenye magazeti yanayozalishwa nchini ili kupunguza gharama za magazeti hayo na hivyo kuwezesha upatikanaji wa taarifa muhimu. Pia Serikali imeendelea kutoa watalaam kwaajili ya kutoa elimu na kuhamasisha matumizi sahihi ya teknolojia katika sekta ya habari kama vile matumizi ya akili unde (AI).

Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Uboreshaji wa sheria za Vyombo vya Habari na Mawasiliano ni msingi wa weledi wa uandishi wa Habari”
Viongozi mbali mbali wakiongozwa na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi alialikwa kama mgeni maalum (wa tatu kutoka kushoto).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa akifuatia hotuba katika mkutano wa Pili wa Mtandao wa Mabaraza Huru ya Habari Afrika (NIMCA), uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC, Arusha.

No comments:

Powered by Blogger.