LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wateja walia kulizwa na biashara mtandaoni

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wateja wa kampuni ya Kim China Business wameipa kampuni hiyo muda wa siku saba kuanzia Jumamosi Agosti 02, 2025 kuhakikisha inawafikishia mizigo waliyoagiza ama kuwarejeshea fedha zao ili kuepuka hatua zaidi za kisheria.

Wateja hao kutoka jijini Mwanza wamesema waliagiza bidhaa mbalimbali ikiwemo simu kupitia kampuni hiyo ya jijini Dar es salaam lakini tangu mwezi Novemba 2024 hawajapokea mizigo yao.

Upande wa kampuni hiyo umewataka wateja hao kufika katika ofisi zake zilizopo Madale jijini Dar es salaam wakiwa na nambari za kuagizia bidhaa zao (orde number) ili kushughulikiwa madai yao.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.