LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWENGE WA UHURU WAZINDUA KLABU YA WAPINGA RUSHWA SHULE YA MSINGI NYANZA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenge wa Uhuru umezindua Klabu ya Wapinga Rushwa katika Shule ya Mchepuo wa Kiingereza Nyanza (Nyanza English Medium School), katika Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Pia Mwenge huo umezindua rasmi mradi wa ujenzi wa vyumba 11 vya madarasa vya ghorofa katika Shule hiyo vilivyojengwa kwa thamani ya shilingi Milioni 659.48 katika shule hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Ismail Ally Ussi ameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo huku akipongeza kuanzishwa Klabu ya Wapinga Rushwa shuleni hapo.

Amesema wanafunzi wa shule hiyo kupitia elimu wanayopewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), tayari ni mabalozi wazuri wa kupinga na kuzuia rushwa katika jamii.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Wapinga Rushwa katika shule hiyo, Raymond Mtemi amesema kupitia klabu hiyo wamejifunza madhara ya rushwa ikiwa ni pamoja na kuminya haki kwa wananchi hivyo wako tayari kuelimisha jamii kuanzia ngazi ya familia kuepuka kutoa ama kupokea rushwa.

Aidha Mwenge huo umezindua Klabu ya Kuzuia Matumizi ya Dawa za Kulevya shuleni hapo yenye lengo la kuwajengea uelewa wanafunzi kutambua madhara ya dawa hizo yakiwemo ya kiafya na kiuchumi.

No comments:

Powered by Blogger.