MWENGE WA UHURU WAWASILI WILAYANI NYAMAGANA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenge wa Uhuru umewasili katika Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Jumatatu Agosti 25, 2025 ukitokea wilayani Ukerewe ambapo mapokezi yake yamefanyika uwanja wa Nyamagana.
Akipokea Mwenge huo, Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi amesema miradi saba itapitiwa ikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 50 ikiwemo maji, vizimba vya samaki, elimu, barabara, afya, usalama wa wananchi na maeneo ya umma.
Pia Makilagi amewahimiza wananchi kujiandaa kushiriki Uchaguzi Mkuu Agosti 29, 2025 kwa amani kama kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru 2025 inavyosisitiza " Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu".
Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ismail Ally Ussi amesema ametoa pongezi wa viongozi wilayani Nyamagana wakiongozwa na DC Amina Makilagi akisema anaamini miradi itakayopitiwa na Mwenge imetekelezwa kwa kiwango bora.
No comments: