LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Nyamagana aongoza hamasa ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2025

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi ameongoza makundi mbalimbali kufanya mazoezi ya viungo na mbio za polepole (jogging), ikiwa ni hamasa kuelekea mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2025.

Makilagi ameongoza mazoezi hayo Jumamosi Agosti 16, 2025 na kutumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Nyamagana Agosti 25, 2025 kwa ajili ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea wilayani Ukerewe.

Amesema Mwenge wa Uhuru 2025 ukiwa katika Wilaya ya Nyamagana utatembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo huku ujumbe kwa mwaka huu ukiwa ni "jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025, kwa Amani na Utulivu.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi (katikati) akiongoza mazoezi ya hamasa kwa ajili ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2025.
Wananchi na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi wakiwa kwenye mazoezi katika mitaa ya Jiji la Mwanza ikiwa ni hamasa kuelekea mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2025.
Wananchi na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi wakiwa kwenye mazoezi katika mitaa ya Jiji la Mwanza ikiwa ni hamasa kuelekea mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2025.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akiwa na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza (kulia) pamoja na wananchi waliojitokeza kwenye mazoezi ya hamasa kuelekea mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2025.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.