LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA Mwanza wapewa mafunzo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) Mkoa wa Mwanza, wamepewa mafunzo ya kuwajengea uelewa zaidi ili kutekeleza kwa weledi majukumu yao.

Akihitimisha mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza Agosti 13, 2025- Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo, Yassin Ally amesema utekelezaji wa MTAKUWWA awamu ya kwanza umesaidia kupunguza vitendo vya ukatili mkoani Mwanza.

Amesema lengo sasa ni kuhakikisha wanaimarisha mifumo ya ulinzi na usalama ili kudhibiti matukio ya ukatili kabla hayajatokea ikiwa ni moja ya malengo ya utekelezaji wa MTAKUWWA awamu ya pili.
Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya MTAKUWWA Mkoa wa Mwanza, Yassin Ally akititimisha mafunzo kwa wajumbe wa kamati hiyo, Ijumaa Agosti 15, 2025.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.