POLISI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI, KUTENDA HAKI
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda ameagiza jeshi la polisi kuhakikisha linatekeleza majukumu yake kwa weledi huku likitenda haki na uwajibikaji kwa wananchi.
Mtanda alitoa agizo hilo Jumatano Agosti 20,2025 wakati akiweka jiwe la msingi katika Kituo kipya cha Polisi Nyegezi jijini Mwanza.
Alisema jeshi la polisi lazima lilinde haki za wananchi ili watoe ule mtazamo wa kuwa kuingia polisi ni bure, ili kutoka ni gharama – suala ambalo limekuwa likichafua sifa ya jeshi hilo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba alitumoa fursa hiyo kuwashukuru wananchi kwa kushiriki ujenzi wa kituo hicho kitakachosaidia kuimarisha ulinzi na kusogeza huduma karibu yao.
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP, Gidion Msuya alisema wajibu wa jeshi la polisi ni kulinda raia na mali zao huku likiimarisha ulinzi na usalama. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda.
No comments: