LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkakati endelevu wa kampuni ya Barrick wafanikisha kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Mining Corporation Mark Bristow - Picha kutoka Maktaba
Toronto- Kampuni ya Madini ya Barrick (NYSE:B)(TSX:ABX) imefanya mkutano wa mwaka kutoa mrejesho wa mkakati wake endelevu,unaojumuisha ushirikiano wake na wadau ukijikita kuhusu utekelezaji wa mkakati endelevu na vipaumbele.Mkutano huo wa kimtandao unafuatia ripoti ya kina ya Mkakati Endelevu ya mwaka 2024 iliyotolewa karibuni ambayo inaonyesha mafanikio muhimu katika uendeshaji wa shughuli za Barrick katika mataifa mbalimbali duniani.

Kampuni inaendelea kuendeleza miradi ya ukuaji wa msingi iliyoundwa kuleta thamani ya muda mrefu kwa wadau wote kupitia ushirikiano wa kweli. Vipaumbele vya uendelevu vya Barrick ni pamoja na kutoa ripoti ya kina ya   utekelezaji  Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs), kudumisha dhamira yake isiyoyumba ya usalama mahali pa kazi, na kuchukua tahadhari za matukio ya mbele na  udhibiti wa uchafuzi wa hali ya hewa kutokana na shughuli zake.

"Mkakati wetu wa uendelevu sio tu mfumo - ni jinsi tunavyounda athari za kudumu, zinazowajibika,"alisema rais wa Barrick na Afisa Mtendaji Mkuu Mark Bristow. "Uchimbaji madini ukifanyika kwa umahiri ni nguvu kubwa ya kuleta maendeleo. Jamii zinazoishi kwenye maeneo ya shughuli zetu zikipata mafanikio  ni mafanikio kwetu pia .”

Muhtasari wa yaliyomo katika ripoti mpya ya utekelezaji mkakati endelevu

Barrick imetoa muhtasari wa ripoti ya utekelezaji wa mkakati endelevu ili kuwawezesha wadau kupata taarifa jinsi kampuni inavyotekeleza  mkakati endelevu, na athari zake katika kuleta mabadiliko chanya.

"Wakati Ripoti ya utekelezaji wa masuala endelevu  ya 2024 ni ya kina na tunatambua umuhimu wa kutoa taarifa muhimu, mazingira ya kuripoti yamebadilika hivi kwamba ripoti hizi zinaendelea kujumuisha mambo mengi ili kukidhi matarajio mbalimbali," alisema Bristow. "Muhtasari wa Ripoti yetu mpya unatoa maelezo ya wazi na yanayoweza kueleweka ya jinsi tunavyofanya kazi katika maeneo yetu yote ya kazi  - kutoka Afrika hadi Marekani, Papua New Guinea hadi Peru – mgao wa faida za uchimbaji madini, kuweka wafanyakazi salama, kulinda mazingira asilia na kutoa thamani inayoonekana, ya kudumu ya kijamii na kiuchumi."

Ripoti ya muhtasari inaangazia athari zinazoweza kupimika na inajumuisha utekelezaji wa mkakati endelevu wa Barrick katika kipindi cha miaka sita tangu muungano uliounda Barrick ya sasa.

Mafanikio muhimu endelevu yaliyopatikana katika kipindi hiki ni kampuni kuwekeza katika matumizi ya nishati safi na matumizi ya vyanzo vya nishati mbadala, usambazaji wa zaidi ya dola bilioni 70 kwa wafanyakazi, biashara katika maeneo yake ya kazi, miradi ya jamii na serikali, na kuunda ushirikiano na jamii zinazoishi jirani na maeneo yake ya kazi  ili kujenga shule, vituo za afya, upatikanaji wa maji safi ya kunywa na miundombinu mingine muhimu - pamoja na uwekezaji katika kuwezesha upatikanaji wa walimu bora, wauguzi na vifaa vinavyohitajika kuboresha upatikanaji wa huduma hizi.

Utoaji wa Ripoti  ya utekelezaji mkakati Endelevu kwa njia ya mtandao na muhtasari wa ripoti hii unaimarisha dhamira ya Barrick ya kutoa taarifa za utendaji wake kwa uwazi na ushirikishwaji wa wadau huku kampuni ikiendelea kuendeleza mkakati wake wa endelevu katika maeneo yake ya kazi sehemu mbalimbali duniani.

No comments:

Powered by Blogger.