Wananchi wahimizwa kutembelea banda la TPHPA kwenye Maonesho ya Nanenane
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Kanda ya Ziwa imeshiriki Maonesho ya Wakulima, Wafugani na Wavuvi maarufu kama Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki katika uwanja wa Nyamhongongolo jijini Mwanza.
Kitaifa maonesho ya Nanenane yanafanyika jijini Dodoma huku pia Kanda mbalimbali zikiandaa maonesho hayo ambapo mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera inashiriki maonesho hayo jijini Mwanza ikiwa ni Kanda ya Ziwa Mashariki.
Meneja wa TPHPA Kanda ya Ziwa, Mary Leina amewahimiza wananchi kutembelea banda la mamlaka hiyo katika uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza ili kupata elimu mbalimbali kuhusu mimea na viuatilifu.
Maonesho ya Nanenane yalianza Agosti Mosi 2025 ambapo kilele ni Ijumaa Agosti 08, 2025 ambapo kwa Kanda ya Ziwa Mashariki ufunguzi rasmi ulifanyika Jumapili Agosti 03, 2025, mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba.
Kaulimbiu ya maonesho ya mwaka huu 2025 ni "chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi".
Meneja wa TPHPA Kanda ya Ziwa, Mary Leina (wa pili kulia) akipokea na kuonyesha ndege isiyo na rubani (Drone) inayotumika kwenye uchunguzi mimea na mazao mbalimbali katika mashamba makubwa.
Meneja wa TPHPA Kanda ya Ziwa, Mary Leina (wa pili kulia) akipokea na kuonyesha ndege isiyo na rubani (Drone) inayotumika kwenye uchunguzi mimea na mazao mbalimbali katika mashamba makubwa.
Meneja wa TPHPA Kanda ya Ziwa, Mary Leina (wa pili kulia) akiwa na watumishi wa mamlaka hiyo kwenye maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki yanayofanyika katika uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza.
Mtumishi wa TPHPA akifurahia jambo.
Meneja wa TPHPA Kanda ya Ziwa, Mary Leina (wa kwanza kushoto) akiwa na watumishi wa mamlaka hiyo kwenye maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki yanayofanyika katika uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza.
No comments: