Wastaafu wakumbushwa kuboresha taarifa zao PSSSF
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wastaafu wanaopokea pensheni kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), wamekumbushwa kuboresha taarifa zao ndani ya miezi mitatu baada ya kustaafu ikiwa majina yao yanatofautiana na yaliyo kwenye kitambulisho cha Taifa NIDA.
Maboresho hayo yanawahusu ambao pia wakati wa utumishi walikuwa wanatumia majina mawili huku vitambulisho vyao vya NIDA vikiwa na majina matatu hivyo ili kuepuka usumbufu ni vyema kufika PSSSF kuboresha taarifa hizo.
Akizungumza kwenye Maonesho ya 32 ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki yanayofanyika uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza, Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande amesema maboresho hayo yatasaidia wastaafu kupata mafao yao kwa wakati bila usumbufu huku pia kudhibiti udanganyifu.
“Mabadiliko haya yatasaidia kudhibiti udanganyifu, kuepuka utofauti wa taarifa za mstaafu baina ya mfuko na taasisi inazoshirikiana nazo” alisema CPA. Kinande huku akitoa rai kwa wastaafu kuhakikisha taarifa zao zinakuwa siri kwani baadhi ya watu huzitumia kufanya utapeli ikiwa zitaachwa wazi.
CPA Kinande aliwakumbusha wastaafu kutopoka maelekezo yoyote kutoka kutoka kwa watu wasiowafahamu ba ikiwa kuna changamoto ni vyema kufika kwenye ofisi za PSSSF zilizo katika mikoa na Kanda mbalimbali nchini ili kupata huduma huku wakiwahimiza kutumia Maonesho ya Nanenane kutatua ama kuboresha taarifa zao.
Maonesho ya Nanenane yalianza Agosti Mosi 2025 ambapo kilele ni Ijumaa Agosti 08, 2025 ambapo kwa Kanda ya Ziwa Mashariki ufunguzi rasmi ulifanyika Jumapili Agosti 03, 2025, mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande (kushoto) akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba (mwenye kofia) alipotembelea banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mwanza.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande akisalimiana na Karibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Elikana Balandya kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mwanza.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki yanayofanyika uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba alipotembelea banda la taasisi hiyo.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba alipotembelea banda la taasisi hiyo.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande akimsaidia mwanachama wa mfuko huo kuhakiki taarifa zake kwa njia ya kidigitali.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande akiwa na watumishi mbalimbali wa mfuko huo wakitoa huduma kwa wanachama kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mwanza.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande akishuhudia huduma zinazotolewa na mfuko huo kwa wanachama wake kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mwanza.
Mwanachama wa PSSSF wakipata huduma kwenye banda la mfuko huo.
Wanachama wa PSSSF wakipata huduma kwenye banda la mfuko huo.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande (kulia) akitoa ufafanuzi kwa mwanachama wa mfuko huo.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande (kushoto) akiteta jambo na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSSF) Kanda ya Ziwa, Emmanuel Kahenda.
Wanachama wa PSSSF wakipata huduma kwenye Maonesho ya Nanenane jijini Mwanza.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Ummy Wayayu aliyetembelea banda la mfuko huo.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi.
Wafanyakazi wa PSSSF wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA. Rajabu Kinande (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki yanayofanyika uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza.
No comments: