LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mpina aikacha CCM, ahamia ACT Wazalendo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, Luhaga Joelson Mpina amejiunga rasmi na Chama cha ACT Wazalendo na amesajiliwa kupitia mfumo wa kidijitali wa chama hicho ujulikanao kama ACT Wazalendo Kiganjani.

Mpina amejiunga na ACT Wazalendo na kusajiliwa na Kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu ambaye amemkaribisha rasmi Mpina na kumpa hadhi ya kuwa mwanachama wa chama hicho chenye mwelekeo wa kijamaa na kidemokrasia.
Mpina alijitosa kuwania tena nafasi yake ya ubunge lakini jina lake halikurejea.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu (kushoto), akimchukua picha aliyekuwa mbunge wa Kisesa mkoani Simiyu, Luhaga Mpina (kulia) kwa ajili ya kumsajilia kitambulisho cha uanachama.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Dorothy Semu, akimsajili Luhaga Joelson Mpina katika Mfumo wa ACT Wazalendo Kiganjani na kuwa mwanachama rasmi wa ACT Wazalendo.

No comments:

Powered by Blogger.