LIVE STREAM ADS

Header Ads

TWENZETU! Maonesho ya Nanenane 2025 kumenoga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki yamekuwa na mwitikio mzuri ambapo wananchi na wadau mbalimbali wanatoa na kupokea elimu kuhusu masuala ya kilimo, ufugaji na uvuvi.

Maonesho hayo yalianza Agosti Mosi 2025 ambapo kilele ni Ijumaa Agosti 08, 2025 ambapo kwa Kanda ya Ziwa Mashariki ufunguzi rasmi ulifanyika Jumapili Agosti 03, 2025, mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba.

Huduma mbalimbali zinatolewa na taasisi za umma na binafsu huku wajasiriamali nao wakiuza bidhaa mbalimbali. Kaulimbiu ya maonesho ya mwaka huu 2025 ni "chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi".
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.