MIRADI YA BILIONI 27 KUPITIWA NA MWENGE WA UHURU ILEMELA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Ismail Ally Ussi amewapongeza viongozi wilayani Nyamagana kwa kutekeleza vyema miradi ya maendeleo.
Ussi ametoa pongezi hizo wakati Mwenge wa Uhuru ukikabidhiwa wilayani Ilemela ukitokea wilayani Nyamagana.
Amesema miradi yote minane yenye thamani ya ya zaidi ya shilingi bilioni 50 iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru imetekelezwa kwa ubora chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba.
Akipongea pongezi hizo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi amesema Mwenge wa Uhuru umeacha alama ya upendo na matumaini kwa wananchi na kwamba wako tayari kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa amani na usalama.
Akipongea Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amir Mkalipa amesema miradi tisa yenye thamani ya shilingi Bilioni 27.6 itapitiwa na Mwenge wa Uhuru wikayani humo.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: