MWENGE WA UHURU WAKOSHWA NA MIRADI YA MAENDELEO NYAMAGANA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenge wa Uhuru umewasili katika Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Jumatatu Agosti 25, 2025 ukitokea wilayani Ukerewe ambapo mapokezi yake yamefanyika uwanja wa Nyamagana.
Akipokea Mwenge huo, Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi amesema miradi saba itapitiwa ikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 50 ikiwemo ya maji, vizimba vya ufugaji samaki, ubarabara, afya, nishati safi ya kupikia, usalama wa wananchi na bustani ya wazi ya Kemondo kwa ajili ya umma.
Pia Makilagi amewahimiza wananchi kujiandaa kushiriki Uchaguzi Mkuu Agosti 29, 2025 kwa amani kama kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru 2025 inavyosisitiza " Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu".
Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ismail Ally Ussi amesema ametoa pongezi wa viongozi wilayani Nyamagana wakiongozwa na DC Amina Makilagi.
Katika Shule ya Msingi ya Mchepuko wa Kiingereza Nyanza, Mwenge wa Uhuru umezindua vyumba 11 vya madarasa vilivyojengwa kwa mfumo wa ghorofa vyenye thamani ya shilingi milioni 659.48 pamoja na Klabu ya Wapinga Rushwa na Dawa za Kulevya.
Miradi mingine iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru ni Kituo kipya cha Polisi Nyegezi, Kituo cha Afya Mkolani huku ukikagua mradi wa Kituo cha Kusukuma Maji Sahwa unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA).
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi (kulia) akizungumza wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025, Ismail Ally Ussi (katikati) akizungumza baada ya kukagua Kituo cha Polisi Nyegezi.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: