MWENGE WA UHURU WAWASILI MKOANI MWANZA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Jumapili Agosti 24, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda, ameupokea Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa shule ya msingi Muluseni wilayani Ukerewe ukitokea mkoani Mara.
Mhe. Mtanda amebainisha kuwa mwwnge huo utakimbizwa kwa siku nane mkoani Mwanza katika miradi 57 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 100.
Amefafanua kuwa katika miradi hiyo 57, 11 itawekewa mawe ya Msingi ikiwa na thamani ya Tshs. 36,879,656,520.00 miradi 30 thamani ya Tshs. 12,978,562,557.50 itazinduliwa ambapo 10 yenye thamani ya shs. 2,475,460,130.90 itafunguliwa na miradi 9 yenye thamani ya Tsh.48,632,209,710.00 itakaguliwa.
Amebainisha kuwa Mwenge wa Uhuru mkoani humo utakimbizwa umbali wa kilometa 722 katika eneo la nchi kavu na majini (nautical mile) 45 katika miradi iliyo kwenye sekta za maji, barabara/madaraja, elimu na afya.
Maeneo mengine ametaja kuwa ni kwenye huduma za kiutawala, kijamii na kiuchumi kwa maendeleo ya wananchi na utawala bora, uhifadhi wa mazingira na utumiaji wa nishati safi na salama, usafi na utunzaji wa masoko na kuzuia na kudhibiti na kuzuia vitendo vya ukatili.
Kadhalika, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa 2025 kwa amani na utulivu kama ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru usemavyo “JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 KWA AMANI NA UTULIVU”.
Katika wakati mwingine, Mkuu wa Mkoa amemkabidhi mwenge wa uhuru Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Mhe. Christopher Ngubiagai kwa ajili ya kuukimbiza katika miradi 8 ya maendeleo leo Agosti 24, 2025.
Mkoa wa Mwanza baada ya kukimbiza mwenge wa uhuru kwa siku nane utakabidhiwa Mkoani Geita katika viwanja vya shule ya sekondari ya Lwezera wilayani Geita.
No comments: