RAIS SAMIA KUJENGA KITUO KIKUBWA CHA KUSAMBAZIA UMEME NCHINI - DKT. BITEKO
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kubwa ya mfano katika sekta ya Nishati.
Biteko amesema kupitia kazi hiyo, Mkoa wa Dodoma muda si mrefu utakuwa ni kitovu cha usambazaji umeme katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Singida, Shinyanga, Tabora, Kigoma na Arusha.
Amesema na kitajengwa kituo kikubwa cha kusambaza umeme na kusimamia gridi ya Taifa.
Aidha Dkt. Biteko amebainisha kuwa hatua iliyopo sasa afari ni kuhakikisha minada yote nchini inatumia nishati safi ya kupikia, ambapo safari hiyo imeanzia katika Mnada wa Msalato jijini Dodoma.
Alhamisi tarehe 21 Agosti 2025, Dkt. Biteko amegawa majiko banifu kwa Mamalishe takriban 27 wanaohudumu katika mnada huo pamoja na majiko ya kuchomea nyama ikiwa ni jitihada za kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia isiyo na madhara kiafya na kimazingira.
No comments: