BODI YA WAKURUGENZI TBS YATEMBELEA JENGO LA 'VIWANGO HOUSE' MWANZA
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Prof. Othman Chande imekagua mradi wa ujenzi wa jengo la maabara na ofisi za taasisi hiyo Kanda ya Ziwa unaotekelezwa eneo la Kiseke jijini Mwanza.
Akizungumza Jumatano Agosti 20, 2025 baada ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa jengo la 'Viwango House', Prof. Chande amenuagiza mkandarasi ambae ni kampuni ya CJIC kutoka nchini China kuongeza kasi ya ujenzi ili mradi huo ukamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
"Baada ya ukaguzi tumeridhika na ubora wa utekelezaji wa mradi huu, kwa sasa tunasisitiza mkandarasi aongeze kasi ili mradi ukamilike kwa wakati" amesema Profesa Chande.
Prof. Chande ameongeza kuwa ujenzi wa maabara na ofisi za TBS katika Kanda mbalimbali nchini ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha huduma inasogezwa karibu na wananchi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Katunzi amebainisha kuwa kukamilika kwa jengo hilo kutaondoa adha ya muda na gharama kubwa za kusafirisha sampuli kwa ajili ya vipimo kwenda Dar es salaam.
"Kwa sasa sampuli zinaenda katika maabara ya Dar es salaam lakini lengo ni kuwa na maabara katika Kanda na hivi karibuni tutakuwa na maabara Dodoma ambapo ujenzi umefikia asilimia 84 na Arusha tunatarajia kuanza ujenzi" amebainisha Dkt. Katunzi.
Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka kampuni ya Kiota Architects, Arch. Chris Olomi amesema mradi umefika asilimia 47.7 ambapo ulianza mwaka 2024 ukitarajiwa kukamilika Aprili 04, 2026 kwa gharama ya shilingi bilioni 12 ikiwa ni jengo la ghorofa sita kwa kuanzia chini ya ardhi (ground floor).
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS, Prof. Othman Chande akizungumza wakati wa ukaguzi wa jengo la maabara na ofisi za TBS Kanda ya Ziwa lililopo Kiseke jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS, Prof. Othman Chande (wa pili kulia) akizungumza na wanahabari baada ya ukaguzi wa jengo la TBS Kanda ya Ziwa. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu TBS, Dkt. Ashura Katunzi.
Meneja wa mradi jengo la TBS Kanda ya Ziwa, Arch. Chris Olomi (kulia) akizungumza na wanahabari.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS, Prof. Othman Chande akisalimiana na mkandarasi baada ya kuwasili katika mradi wa ujenzi wa maabara na ofisi za TBS Kanda ya Ziwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS Prof. Othman Chande (wa tatu kulia) na Mkurugenzi Mkuu TBS Dkt. Ashura Katunzi (wa pili kulia) wakisalimiana na wakandarasi baada ya kuwasili katika mradi wa ujenzi wa maabara na ofisi za TBS Kanda ya Ziwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS Prof. Othman Chande (katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu TBS Dkt. Ashura Katunzi (kushoto). Kulia ni Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa, Happy Brown.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS Prof. Othman Chande na viongozi alioambatana nao wakipata maelezo kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa jengo la TBS Kanda ya Ziwa (Viwango House).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS Prof. Othman Chande (katikati) na viongozi mbalimbali alioambatana nao wakipata maelezo kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa jengo la TBS Kanda ya Ziwa (Viwango House).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TBS Prof. Othman Chande (katikati) na viongozi mbalimbali alioambatana nao wakipata maelezo kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa jengo la TBS Kanda ya Ziwa (Viwango House).
Viongozi wa TBS wakiteta jambo wakati wa ukaguzi wa mradi wa Viwango House.
Muonekano wa jengo la TBS Kanda ya Ziwa (Viwango House) ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 47.7.
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: