LIVE STREAM ADS

Header Ads

Tanfoam Marathon Yazindua Mbio Kamili za Km 42, Wakaribisha Washiriki wa Kimataifa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Rais wa RT, Rogath John Stephen (wa kwanza kulia) akionyesha kits zitakazotimika katika msimu wa pili wa mbio za tanfoam marathon desemba 7,2025 baada ya uzinduzi iliyofanyika jijini Arusha, anaefuata ni mwenyekiti wa maandalizi ya mbio hizo Glorious Temu na mwenyekiti wa ARAA Gerald Babu.
Rais wa RT, Rogath Stephen (wa pili kulia) akiwakabidhi kits baadhi ya mawakala wauzaji wa vifaa vya mbi za Tanfoam Marathon.

Na Mwandishi Wetu, Arusha.

Waratibu wa mbio ndefu za Tanfoam Marathon wamefungua rasmi milango kwa ajili ya kuruhusu wanariadha kutoka mataifa mbalimbali duniani kushiriki mbio hizo kwa msimu wa pili.

Mbio hizo zinazotarajia kufanyika nchini desemba 7, 2025, kwa mara ya kwanza zitakuwa na umbali wa kilomita 42 huku zingine za kilomita 21, 10 na tano zikiendelea.

Mwenyekiti wa maandalizi wa mbio hizo, Glorious Temu amesema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa mbio hizo msimu wa pili iliyokwenda sambamba na kutambulisha jezi zitakazotumika na ramani ya njia ya kukimbia.

Temu amesema kuwa mbio hizo zitakimbiwa na wanariadha wasiozidi 1500 kutoka mikoa mbalimbali nchini na mataifa ya nje.

“Kwa mwaka huu tumefanya maboresho makubwa ikiwemo kuongeza masafa kamili ya mbio ndefu (Kilomita 42) lakini pia kuongezea usajili wa hadhi ya kimataifa hivyo kuruhusu wanariadha kutoka mataifa ya nje kushiriki”

Amesema kuwa maandalizi yote kuelekea mbio hizo zinaendelea ikiwemo kuboresha zawadi iwe zaidi ya milioni 30 walizotoa mwaka jana.


Rais wa RT, Rogath Stephen (wa pili kulia) akiwakabidhi kits baadhi ya mawakala wauzaji wa vifaa vya mbi za Tanfoam Marathon.

Amesema malengo makubwa ya mbio hizo ni kuinua vipaji vya riadha na kutangaza nchi kama kitovu cha maendeleo ya michezo, utalii.

Ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wanariadha wote wa kitaifa na kimataifa kujiandikisha katika vituo vyao vya maduka ya mauzo ya magodoro ya Tanfoam lakini katika klabu za mazoezi na ndani ya viwanja vya sheikh amri abeid Arusha.

Akizundua mbio hizo, Rais wa shirikisho la riadha Tanzania(RT), Rogath John Stephen amewapongeza waandaaji wa mbio hizo kwa kufuata taratibu zote zilizoainishwa za kuendesha mbio yao kwa msimu huu.
Rogath ametumia nafasi hiyo kuwajulisha waandaji wote wa mbio nchini juu ya kanuni mpya za shirikisho zilizoandaliwa ikiwemo za kuwataka kujumuisha kwa lazima mbio za watoto.

“Tumekuwa tukiwaunganisha watoto wadogo kukimbia na watu wazima tena kilomita 10, jamani tunawadumaza, hawa watoto ndio maana TR imefikia mahali na kusema hapana na lazima mbio yoyote iwe na tukio la watoto”amesema na kuongeza;

“Hii si yetu bali ni kwa mujibu wa shirikisho la riadha duniani ambao wanataka kuwa na kipengele cha mbio za watoto peke yao na zawadi yao kama motisha na sisi imefika wakati kuanzia mwakani tutasimamia hilo” amesema.

Amesema kuwa hiyo itasaidia kuondoa mateso kwa watoto lakini pia kuupenda mchezo na mbali zaidi kutengeneza kizazi chenye warithi wa mabingwa wa mchezo huu wa riadha watakaotumika kama akiba ya vipaji.

Amesema kuwa kuanzia mwakani hawatatoa kibali kwa mtu yoyote asie na kipengele hicho, lakini pia hawataruhusu mtu kufanya matangazo bila kibali na zaidi watataka kuona nembo ya shirikisho kwenye matangazo yote ya mbio.

Nae mwenyekiti wa chama cha riadha Mkoa wa Arusha, Gerald Babu amesema kuwa tanfoam marathon imekuwa moja ya mbio bora Arusha ambayo inakuza vipaji lakini pia kusaidia maandalizi ya wanariadha kujiandaa na mashindano ya kimataifa.

“Mbio hizi zimesaidia wanariadha wetu kupata jukwaa la kupima kasi yao lakini zawadi za kifedha zimewapa mtaji wa kujiandaa na mbio zingine za kimataifa kwa ajili ya kuitangaza nchi hivyo tutoe rai kwa waandaji wengine wawe wanatoa zawadi nono kusaida wanariadha kupunguza makali ya gharama za mchezo huu.”

No comments:

Powered by Blogger.