YAWE, TRA NA MANISPAA YA SHINYANGA WATOA ELIMU YA KODI KWA WAJASIRIAMALI
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Afisa wa Kodi kutoka TRA Shinyanga, Semeni Mbeshi, akitoa elimu kuhusu mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mwaka 2025/2026,wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali Manispaa ya Shinyanga kuhusu umuhimu wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara

Mratibu wa Mradi wa “Kijana Wajibika, Ijue Kodi Yako, Lipa na Shiriki” kutoka Shirika la YAWE, Peter Nampala akizungumza wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali Manispaa ya Shinyanga kuhusu umuhimu wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara

Afisa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara TRA Mkoa wa Shinyanga, Mkoji Wanjala akitoa elimu kuhusu Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la YAWE kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia mradi wa “Kijana Wajibika, Ijue Kodi Yako, Lipa na Shiriki” unaotekelezwa na Shirika la Restless Development kupitia YAWE, limetoa elimu kwa wajasiriamali kuhusu umuhimu wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara.
Dawati hilo limeanzishwa na TRA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali likiwa na lengo la kuwatambua, kuwasikiliza na kuwawezesha wafanyabiashara ili kukuza mitaji na kuongeza tija katika biashara zao.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo Jumanne Septemba 16, 2025 mjini Shinyanga, Mratibu wa Mradi wa “Kijana Wajibika, Ijue Kodi Yako, Lipa na Shiriki” kutoka Shirika la YAWE, Peter Nampala, amesema elimu hiyo itawasaidia wajasiriamali kuijengea uelewa jamii kuhusu masuala ya kodi, kutambua fursa zilizopo na kurasimisha biashara zao.
“Mbali na kutoa elimu ya masuala ya kodi kutoka TRA na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, pia tumepokea mrejesho kuhusu mapendekezo ya kodi kutoka TRA na Halmashauri ikiwa ni pamoja na kodi ya majengo,” amesema Nampala.
Kwa upande wake, Afisa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara TRA Mkoa wa Shinyanga, Mkoji Wanjala, ameeleza kuwa, kuanzishwa kwa dawati hilo ni fursa ya kipekee ya kuimarisha mazingira ya biashara mkoani Shinyanga, hatua itakayosaidia kuongeza mapato ya Serikali, kukuza ajira na kuimarisha uchumi wa wananchi.
Ameeleza kuwa Dawati hilo lina jukumu la kusaidia kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wanaofanya biashara katika sekta isiyo rasmi ili waweze kusajiliwa, kutambuliwa na hatimaye kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali.
“Lengo la Dawati hili ni kuhakikisha kila mfanyabiashara, mdogo, mkubwa, anatambulika rasmi na anapata msaada unaohitajika. Dawati hili litakuwa ni nyenzo muhimu ya kuwafikishia huduma karibu, kutoa elimu ya biashara na kusikiliza changamoto zao,” amesema Wanjala.
Akitoa elimu kuhusu mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mwaka 2025/2026, Afisa wa Kodi kutoka TRA Shinyanga, Semeni Mbeshi, amesema mabadiliko hayo yatasaidia kupanua wigo wa kodi na kuweka mazingira bora zaidi ya ulipaji kodi.
Naye Afisa Biashara Manispaa ya Shinyanga, Victor Kajuna, amesema Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga inaendelea kushirikiana na TRA kuhakikisha kunakuwepo na mazingira rafiki ya ulipaji kodi bila kuwabughudhi wafanyabiashara na wajasiriamali.
Mratibu wa Mradi wa “Kijana Wajibika, Ijue Kodi Yako, Lipa na Shiriki” kutoka Shirika la YAWE, Peter Nampala akizungumza wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali Manispaa ya Shinyanga kuhusu umuhimu wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara - Picha na Kadama Malunde
Mratibu wa Mradi wa “Kijana Wajibika, Ijue Kodi Yako, Lipa na Shiriki” kutoka Shirika la YAWE, Peter Nampala akizungumza wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali Manispaa ya Shinyanga kuhusu umuhimu wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara
Mratibu wa Mradi wa “Kijana Wajibika, Ijue Kodi Yako, Lipa na Shiriki” kutoka Shirika la YAWE, Peter Nampala akizungumza wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali Manispaa ya Shinyanga kuhusu umuhimu wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara
Afisa wa Kodi kutoka TRA Shinyanga, Semeni Mbeshi, akitoa elimu kuhusu mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mwaka 2025/2026,wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali Manispaa ya Shinyanga kuhusu umuhimu wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara
Afisa wa Kodi kutoka TRA Shinyanga, Semeni Mbeshi, akitoa elimu kuhusu mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mwaka 2025/2026,wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali Manispaa ya Shinyanga kuhusu umuhimu wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara
Afisa wa Kodi kutoka TRA Shinyanga, Semeni Mbeshi, akitoa elimu kuhusu mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mwaka 2025/2026,wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali Manispaa ya Shinyanga kuhusu umuhimu wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara
Afisa wa Kodi kutoka TRA Shinyanga, Semeni Mbeshi, akitoa elimu kuhusu mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mwaka 2025/2026,wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali Manispaa ya Shinyanga kuhusu umuhimu wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara
Afisa wa Kodi kutoka TRA Shinyanga, Semeni Mbeshi, akitoa elimu kuhusu mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mwaka 2025/2026,wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali Manispaa ya Shinyanga kuhusu umuhimu wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara
Afisa wa Kodi kutoka TRA Shinyanga, Semeni Mbeshi, akitoa elimu kuhusu mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mwaka 2025/2026,wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali Manispaa ya Shinyanga kuhusu umuhimu wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara
Afisa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara TRA Mkoa wa Shinyanga, Mkoji Wanjala akitoa elimu kuhusu Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara

Afisa Biashara Manispaa ya Shinyanga, Victor Kajuna akitoa elimu kuhusu kodi wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali Manispaa ya Shinyanga kuhusu umuhimu wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara

No comments: