LIVE STREAM ADS

Header Ads

MR. BLACK ATOA TANI 1.5 ZA SARUJI NA VIFAA KWA SHULE 9 SHINYANGA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Vifaa na Mahitaji ya Shule za Msingi na Sekondari Vilivyotolewa na BSL kwa Ajili ya Kuendeleza Elimu katika Manispaa ya Shinyanga
Makabidhiano ya vifaa na mahitaji ya shule yakiendelea 
Mkurugenzi wa The BSL Investments Company Limited na mwanzilishi wa BSL Schools Tanzania na Rwanda, Ndugu Peter Frank Lugumi (maarufu kama Mr. Black), ameendelea kuthibitisha dhamira yake ya kusaidia sekta ya elimu kwa vitendo baada ya kukabidhi msaada mkubwa wa vifaa kwa shule za msingi tisa (9) katika Manispaa ya Shinyanga.

Mr. Black ametoa msaada huo leo Oktoba 3,2025, ambapo pia alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya darasa la saba ya Shule ya Msingi Ibinzamata, akitumia tukio hilo kama fursa ya kuunga mkono jamii yake kupitia programu za Uwajibikaji wa Jamii wa Kampuni (CSR).

Katika mchango huo, Mr. Black ametoa tani moja na nusu ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa madarasa, ujenzi wa ukuta na vyoo katika shule za msingi Kambarage, Nhelegani na Town.

Vilevile, amekabidhi seti za jezi kamili kwa shule za msingi Bugayambelele, Kizumbi na Ibinzamata pamoja na mipira minne (4) ya mpira wa miguu kwa ajili ya shule nne.

Kwa upande wa miundombinu ya ofisi za walimu, ametoa viti 15 kwa shule za msingi Kitangiri, Ibinzamata, Ushirika na Mapinduzi B.

Aidha, shule ya msingi Kizumbi imenufaika na tripu mbili (2) za mchanga, huku shule za msingi Bugoyi na Mapinduzi B zikikabidhiwa ndoo za rangi kwa ajili ya uboreshaji wa madarasa.

 Pia, kwa kuthamini walimu, Mr. Black ametoa unga wa ngano kwa ajili ya chai ya walimu katika shule ya msingi Ibinzamata.

Jumla ya msaada huo una thamani ya Shilingi 3,857,000/=, hatua inayodhihirisha dhamira ya BSL katika kuboresha mazingira ya elimu na kufanikisha upatikanaji wa miundombinu bora kwa walimu na wanafunzi.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Mr. Black amewaasa wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana na serikali na jamii katika kuunga mkono maendeleo ya elimu mkoani Shinyanga.

Kwa upande wao, Afisa Mtendaji wa Kata ya Kitangiri, Bi. Adela Mkinga, pamoja na Afisa Elimu Kata ya Ibinzamata, Bi. Juliana Limbe, wameishukuru BSL kwa msaada huo, wakibainisha kuwa utakuwa chachu ya kuinua kiwango cha elimu na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa watoto wa Shinyanga.
Vifaa na Mahitaji ya Shule za Msingi na Sekondari Vilivyotolewa na BSL kwa Ajili ya Kuendeleza Elimu katika Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa BSL, Peter Frank akizungumza wakati akikabidhi Vifaa na Mahitaji ya Shule za Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa BSL, Peter Frank akizungumza wakati akikabidhi Vifaa na Mahitaji ya Shule za Manispaa ya Shinyanga
Makabidhiano ya vifaa na mahitaji ya shule yakiendelea kati ya BSL na viongozi wa elimu wa Manispaa ya Shinyanga 
Makabidhiano ya vifaa na mahitaji ya shule yakiendelea 
Makabidhiano ya vifaa na mahitaji ya shule yakiendelea 
Makabidhiano ya vifaa na mahitaji ya shule yakiendelea 
Makabidhiano ya vifaa na mahitaji ya shule yakiendelea 
Makabidhiano ya vifaa na mahitaji ya shule yakiendelea 
Makabidhiano ya vifaa na mahitaji ya shule yakiendelea 
Makabidhiano ya vifaa na mahitaji ya shule yakiendelea 
Makabidhiano ya vifaa na mahitaji ya shule yakiendelea 

Makabidhiano ya vifaa na mahitaji ya shule yakiendelea 
Makabidhiano ya vifaa na mahitaji ya shule yakiendelea.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 

No comments:

Powered by Blogger.