LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIJIJI 11 TARIME KUANZA KUPATA MAJI SAFI YA MRADI WA UPANUZI NYANGOTO UNAOTEKELEZWA KWA FEDHA ZA BARRICK NORTH MARA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Matenki ya maji ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa upanuzi wa chanzo cha mradi utakuwa ukitoa huduma ya kwa vijiji vyote 11 vilivyo ndani ya mgodi wa North Mara
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ismail Ali Ussi, akizindua mradi huu mwezi Agosti mwaka huu

👉Kukamilika mwezi ujao

Upanuzi wa mradi wa maji Nyangoto unaotekelezwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 2.6  zitokanazo na fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) zilizotolewa na mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara katika mji mdogo wa Nyamongo wilayani Tarime upo katika hatua za mwisho ambapo kufikia mwishoni mwa mwezi ujao vijiji saba zaidi vitaanza kupata maji ya uhakika na kwa wakati wote.

Akiongea na Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii (CDC) inayoibua na kusimamia miradi inayotekelezwa kwa fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) zinazotolewa na Mgodi wa Barrick North Mara, Godfrey Kegoye, amesema mradi huu utakuwa umekamilika na kuanza kufanya kazi hadi ifikapo juma la mwisho la mwezi ujao wa Desemba 2025.

Kegoye amevitaja vijiji vitakavyonufaika kwa kupata maji baada ya mradi kukamilika kuwa ni Kewanja, Kerende, Msege, Nyakunguru, Nyamwaga, Genkuru na Komarera. “Utekelezaji wa mradi upo mwishoni, mkandarasi amekwishatandaza mabomba na tunamtaka ahakikishe anaukamilisha kwa wakati,” amesema Kegoye ambaye pia ni Diwani mteule wa kata ya Matongo.

Amesema kabla ya kutekelezwa kwa mradi huu ni vijiji vinne tu katika kata ya Matongo vinavyopata maji ambavyo alivitaja kuwa ni Nyangoto, Mjini Kati, Matongo na Nyabichune. Mradi huu utaondoa kero ya maji ambayo imekuwa ya muda mrefu na huu ni mradi wa kimkakati uliotekelezwa kutokana na fedha zilizotolewa na mwekezaji katika eneo hili”, amesema.

Ameongeza kuwa faida nyingine ya mradi huu ni kwamba utakapokamilika huduma ya maji katika vijiji ambavyo tayari vimefikiwa vitakuwa vikipata huduma ya maji safi kwa saa 24.

Mbali na mradi huu wa maji, amesema ipo miradi mingine mingi na mikubwa ambayo imetekelezwa na inayoendelea kutekelezwa kwa fedha za CSR zinazotolewa na Barrick North Mara katika sekta za elimu, afya na miundombinu ya barabara.

 Pia ameongeza kuwa wakazi wanaoishi jirani na mgodi wananufaika kwa fedha za mrabaha, ajira, ufadhili kwa wanafunzi na fursa za kibiashara kwa wazabuni na wakandarasi wazawa.

Kwa mujibu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazigira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Tarime, utekelezaji wa mradi huo utaongeza uzalishaji kutoka lita 2,314,000 za sasa hadi 10,213,000 na hivyo kufikia lengo la serikali la mwaka 2020-2025 la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi waishio vijijini.

Mradi huo ulizinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ismail Ali Ussi, mwezi Agosti na ulianza kutekelezwa mwezi Februari mwaka huu.

Ufanikisha wa mradi huu ni moja ya utekelezaji wa mkakati endelevu wa kampuni ya Barrick unaojumuisha ushirikiano na wadau na vipaumbele ambao umelenga kufanikisha kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii zinazoishi kwenye maeneo yaliyopo Jirani na migodi yake sambamba na kufanikisha utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Dunia (SDGs).

Ripoti ya utekelezaji Mkakati Endelevu ya mwaka 2024 ya kampuni ya Barrick Mining Corporation iliyotolewa karibuni imebainisha mafanikio muhimu yaliyopatikana katika uendeshaji wa shughuli zake katika mataifa mbalimbali duniani.

Kampuni inaendelea kuendeleza miradi ya ukuaji wa msingi iliyoundwa kuleta thamani ya muda mrefu kwa wadau wote kupitia ushirikiano wa kweli. Vipaumbele vya uendelevu vikiwa ni Pamoja na kutoa ripoti ya kina ya utekelezaji Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs), usalama mahali pa kazi, kuchukua tahadhari ya matukio ya mbele, kulinda mazingira asilia na kutoa thamani inayoonekana ya kudumu ya kijamii na kiuchumi.

Mafanikio muhimu endelevu yaliyopatikana yaliyobainishwa katika ripoti hiyo ni kampuni kuwekeza katika matumizi ya vyanzo vya nishati mbadala,Uwezeshaji biashara katika maeneo yake ya kazi,miradi ya jamii na Serikali, na kuunda ushirikiano na jamii zinazoishi jirani na maeneo yake ya kazi kwa kutekeleza miradi ya kujenga shule,vituo vya afya,upatikanaji wa maji safi ya kunywa na miundombinu mingine muhimu-pamoja na uwekezaji katika kuwezesha upatikanaji wa walimu bora,wauguzi na vifaa vinavyohitajika kuboresha upatikanaji wa huduma hizi.


No comments:

Powered by Blogger.