PSSSF MSHINDI WA KWANZA TUZO ZA UANDAAJI BORA MAHESABU ZA NBAA 2025
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (kulia), akimkabidhi, Mkurugenzi wa Fedha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Neema Kuwite, tuzo ya mshindi wa kwanza ya umahiri katika uaandaji wa taarifa za mahesabu kwa mwaka unaoishia 2024, katika kundi la Hifadhi ya Jamii zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwenye hafla ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam usiku wa Desemba 04, 2025.
***
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetunukiwa tuzo ya mshindi wa Kwanza ya Umahiri katika Uaandaji wa Taarifa za Mahesabu kwa mwaka unaoishia 2024, katika kundi la hifadhi ya jamii, zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Laurent Deogratius Luswetula alimkabidhi Tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Fedha PSSSF, Bi. Neema Kuwite ambaye alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam usiku wa Desemba 04, 2025.
“Tunamshukuru Mungu na tunafurahi sana kwa kupewa hii tuzo, tumeweka muendelezo kama tulivyopata mwaka jana, naishukuru Bodi ya Wadhamini na Menejimenti kwa usimamizi wao mzuri lakini pia watumishi wote kwa ushirikiano na utendaji unaozingatia taaluma” alisema Bi. Kuwite baada ya kupokea tuzo hiyo.
Ushindi huu kwa PSSSF unaonyesha uandaaji wetu wa mahesabu unafuata viwango vya kimataifa vinavyoelekeza namna bora ya kuandaa hesabu katika sekta ya hifadhi ya jamii.
“Tunawahakikishia wadau wetu wote wakiwemo wastaafu kwamba PSSSF ni tulizo la moyo Leo, Kesho Pamoja na kwamba wana uhakika wa kuendelea kupata Mafao yao kwa sababu Mfuko uko imarakabisa” alitoa hakikisho.
Akizunhumza namna washindi walivyopatikana, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno, alisema Jumla ya Tasisi za Umma na Binafsi 86 zilishiriki katika mchakato wa kuwasilisha mahesabu kwa mwaka unaoishia 2024.
“Tunawapa viwango vyetu vya uhasibu na masuala mbalimbali tuliyoyaorodhesha, na ikli ushinde kuna vitu kama 1392 na vingapi umevipata kikamilifu na aliyepata asilimia 75 ndiye anakuwa mshindi. Pia tunaangalia kama umepata hati safi na si vinginevyo” alisema CPA Maneno.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Laurent Deogratius Luswetula, aliwapongeza washindi wote na kuwataka waendelee kuzingatia weledi ili waendelee kuwa washidni an wale walioshindwa kufikia vigezo wametakiwa kujirekebisha ili nao waweze kufanya vizuri.
Mkurugenzi wa Fedha PSSSF, Bi. Neema Kuwite akiwa amebeba tuzo ya mshindi wa Kwanza ya Umahiri katika Uaandaji wa Taarifa za Mahesabu kwa mwaka unaoishia 2024, katika kundi la hifadhi ya jamii, zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), katika hafla ya kutoa tuzo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Desemba 4, 2025.Mkurugenzi wa Fedha PSSSF, Bi. Neema Kuwite (aliyebeba tuzo), akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa PSSSF katika hafla ya utoaji tuzo za Umahiri katika Uaandaji wa Taarifa za Mahesabu kwa mwaka unaoishia 2024, zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). PSSSF ilishinda tuzo hiyo katika kundi la hifadhi ya jamii.


No comments: