LIVE STREAM ADS

Header Ads

KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII AWAASA WANAHABARI KUONGEZA KASI YA KUANDIKA HABARI ZINAZOHUSIANA NA UTALII HAPA NCHINI. ATOA HAMASA KWA WATANZANIA KUUKUZA UTALII WA NDANI.



Katibu Mkuu Wizara ya Mali asili na Utalii Tarish Maimuna
Waandishi wa habari hapa nchini wameaswa kuongeza kasi ya kuandika habari zinazohusiana na vivutio mbalimbali vya Utalii, kwa lengo la kuongeza na kukuza uelewa juu ya umhimu wa Utalii katika jamii, jambo litakalosaidia kukuza Utalii wa ndani na nje hapa nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Tarish Maimuna ameyasema hayo hii leo Mkoani Mwanza, wakati akifungua Mkutano wa Siku Tatu ulioanza leo baina ya Shirika la Hifadhi za Taifa nchini TANAPA na Wahariri wa Vyombo mbalimbali hapa nchini.

“Ili Utalii uweze kukua, hususani Utalii wa ndani jamii ni lazima ipate taarifa sahii Kuhusiana na Vivutio vya Utalii vilivyopo hapa nchini, hivyo wanahabari na Vyombo vya habari kwa ujumla wanapaswa kuongeza kasi katika kuandika habari zinazohusiana na Utalii”.Alisema Maimuna.
Katibu Mkuu Wizara ya Mali asili na Utalii Tarish Maimuna
Kuhusu Utalii wa ndani hapa nchini, amesema kuwa bado hali siyo nzuri hivyo vyombo vya habari viongeze hamasa ya kuhamasisha wanajamii kutembelea vivutio vilivyopo hapa nchini huku akibainisha kwamba pamoja na umhimu wa Utalii wa nje, bado utalii wa ndani unachangia katika utalii endelevu hapa nchini.

Aidha amebainisha kuwa amebainisha kuwa Sekta ya Utalii ni miongoni mwa Setka zinazochangia kwa asilimia kubwa katika uchumi wa Taifa sanjari na Kuongeza upatikanaji wa ajira hapa nchini.

“Mwaka jana pekee Sekta ya Utalii ililiingia Taifa Dolla za Kimarekani Bilioni 1.8 huku ikitoa ajira za moja kwa moja na Zisizo za moja kwa moja zipatazo Milioni Moja, Laki moja Tisini na Tisa elfu ambapo jumla ya Watalii wa nje Milioni Moja, Laki moja thelathini na tano elfu Mia nane themanini na nne”, Alisema Maimuna huku akiongeza kuwa Sekta ya Utalii ni sekta ambayo inaweza kumnufaisha kila mtu katika jamii, mfano mama ntilie ambao hujiajiri katika maeneo ya Utalii.
Kaimu Katibu Tawala Mkoani Mwanza Cresencia Joseph
Azungumza katika Mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu TAPANA, Ibrahim Mussa ambae ni Mkurugenzi wa Utalii na Masoko kutoka TANAPA, alibainisha kuwa Mikutano baina ya TANAPA na wanahabari imekuwa ikiongeza tija katika Sekta ya Utalii hapa nchini ambapo Mkutano wa kwanza ulifanyika mwaka jana Mkoani Iringa na baada ya Mkutano huo habari juu ya Utalii ziliongezeka hadi kufikia asilimia 92.

Aidha alibainisha kuwa bado utalii wa ndani ni changamoto kubwa katika sekta ya utalii hapa nchini kwa kuwa Watanzania wengi hawana desturi ya kutembea vivutio vya utalii hapa nchini, ambapo ameahidi kuwa TANAPA itaendelea kutoa ushirikiano wake ili kufanikisha utalii wa ndani hapa nchini badala ya kutegemea Utalii wan je.
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA Ibrahim Mussa
Wanahabari
Kwa Upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Cresencia Joseph ambae amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika Mkutano huo, alitoa rai kwa washiriki wa Mkutano huo kutoka na maadhimio ya pamoja juua ya nini cha kufanya ili kupambana na Ujangili katika hifadhi za Taifa hapa nchini.

Nao baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo ambao ni baadhi ya Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, waliozungumza nje ya Ukumbi wa Mkutano huo wameeleza kuwa vyombo vya habari vina Mchango Mkubwa wa Kukuza Sekta ya Utalii hapa nchi huku wakibainisha kuwa habari sahihi juu ya Utalii wa ndani bado zinahitajika ili kukuza utalii huo kwa kuwa bado hakuna taarifa sahihi juu ya utalii wa ndani katika jamii.
                                                 
Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Hotel ya JB Belmont Jiji Mwanza umeanza leo Jumatatu na unatarajiwa kutamatishwa Alhamisi ya may 29 wiki hii ambapo pamoja na Mada nyingine, Mada kuu inayojadiliwa inaendana na Kaulimbiu ya mwaka huu inayosema “Wajibu wa Vyombo vya habari katika kuuza Utalii”.

No comments:

Powered by Blogger.