SABABU TATU ZA NDOA YA MH.VICK KAMATA KUYEYUKA.
Vick akiwa amelazwa hospitalini baada ya ndoa yake kuyeyuka |
SABABU ZA KANISA
Habari za ndani
zilidai kuwa kanisa lilibaini upungufu mkubwa kwa bibi harusi na kumwambia ndoa
haitakuwepo. Upungufu huo ni pamoja na Vicky Kamata kushindwa kuwasilisha cheti
chake cha ubatizo, pia hakuwahi kupata kipaimara. Ilidaiwa kuwa vitu hivyo kwa
uchache wake ni kikwazo kikubwa kwa mtu kufikia daraja la Sakramenti ya Ndoa.
SABABU ZA NDANI
Ukiachana na sababu
hizo za kanisa, Ijumaa Wikienda lilichimbua na kubaini sababu kuu 3 ambazo
zilikuwa kisiki cha kufungwa kwa ndoa hiyo.
SABABU YA KWANZA
Kwa mujibu wa
chanzo, mwanaume aliyetaka kufunga ndoa na Vicky ana ndoa nyingine ya kanisa na
imejaliwa kupata watoto kadhaa hivyo isingekuwa rahisi kufungwa kwa ndoa
nyingine kwa mujibu wa maandiko ya Biblia. Mume mmoja mke mmoja mpaka kifo
kiwatenganishe.
MKE ATINGA BUNGENI
Chanzo kilizidi
kudai kuwa wiki iliyopita, mwanamke huyo ambaye jina halikupatikana, alitinga
bungeni na kuonana na Spika wa Bunge, Anne Makinda ambapo alijitambulisha ndiye
mke wa Charles anayetaka kufunga ndoa na Vicky Kamata.
“Mke wa bwana harusi
alikuja Dodoma juzi, akasaidiwa kuonana na spika na mbunge mmoja (jina tunalo).
“Alimwambia spika
yeye ndiye mke wa ndoa wa Charles, ila walitengana. Lakini alisema pamoja na
kutengana huko, ndoa ya Kikristo haifungwi mara mbili labda mmoja afe. Kwa hiyo
mumewe hawezi kufunga ndoa na Vicky,” kilisema chanzo.
SABABU YA PILI
Sababu ya pili
ilielezwa kuwa, Vicky asingeweza kufunga ndoa hiyo kwani mwanaume huyo alishatoa
mahari kwa msichana mmoja (jina tunalo) wa jijini Dar na ukweni anajulikana.
“Alishatoa mahari kwa msichana mwingine mbali na Vicky, ukweni anajulikana”.
“Sasa ilipotoka ile
picha yake kwa mara ya kwanza kwenye Gezeti la Ijumaa (Mei 16, 2014) yenye kichwa
cha habari ndoa ya Vicky itatumia shilingi milioni 96 ikawa kasheshe kwa yule
msichana na ukweni, ndiyo jamaa akaamua kutangaza kubatilisha ndoa na Vicky,”
kilisema chanzo.
SABABU YA TATU
Sababu ya tatu
ilitajwa ni kitendo cha kuumwa. Wikiendi iliyopita, Vicky aliugua ghafla na
kulazwa katika Hospitali ya Tabata General jijini Dar kwa hiyo isingekuwa
rahisi ndoa kufungwa Jumamosi kutokana na hali yake kuwa mbaya.
Vick akiwa nchini China Mwanzo mwa Mwezi huu kwa ajili ya maandalizi ya Harusi |
WAANDISHI WATINGA
HISPITALI
Ijumaa iliyopita,
waandishi wetu walitinga kwenye hospitali hiyo na kukutana na daktari mmoja
ambaye alikiri Vicky kulazwa hapo lakini alikataa waandishi wasimuone kwa
sababu hayuko katika hali nzuri kiafya. “Ni kweli Vicky kalazwa hapa lakini
hamuwezi kumwona, hayuko katika hali nzuri, anahitaji kupumzika jamani, please,”
alisema daktari huyo.
HATIHATI
ILISHAKUWEPO
Katika Gazeti la
Uwazi la Mei 20, 2014 ukurasa wa mbele kulikuwa na habari ndogo yenye kichwa
kisemacho; NDOA YA MIL. 96 YA VICKY KAMATA HATIHATI KUFUNGWA.
Katika habari hiyo
ilielezwa kuwa ndoa hiyo isingefungwa kutokana na kuibuka kwa mizengwe
kibao.
Habari za ndani
zilisema mizengwe hiyo iliibuka katika hatua za mwisho na kusababisha mwanaume
kuamua kubatilisha ndoa hiyo ambayo ilikuwa ifungwe Mei 24, mwaka huu jijini
Dar.
KIONGOZI MKUBWA
SERIKALINI
Ilidaiwa kuwa baada
ya kuibuka kwa zengwe na mume kutangaza ndoa basi, Vicky aliumia na kuzifikisha
habari hizo kwa Spika Makinda ambapo naye alizifikisha kwa kiongozi mmoja
mkubwa serikalini, hasa bungeni.
Kiongozi huyo
alichukua jukumu la kumvutia waya bwana harusi na kumsihi kutochukua mawazo
hayo na ikibidi ndoa ifungwe lakini mwanaume huyo alikataa katakata akisema
mambo hayo ni ya kifamilia zaidi kwa hiyo yaachwe kwenye familia.
MAMA SITTA ASIKITIKA
Habari zinazidi
kusema kuwa kati ya watu ambao wamehuzunishwa na kutofungwa kwa ndoa hiyo ni
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta ambaye
aliposikia kuyeyuka kwa ndoa hiyo alisikitika si kwa sababu alikuwa kwenye
vikao vya harusi, bali pia aliuona wakati mgumu atakaoupata Mhe. Vicky.
Pamoja na yote
yaliyojitokeza, habari zinadai kwamba baadhi ya wabunge waliochanga pesa ili
kufanikisha harusi hiyo tangu juzi wameanza kuulizia michango yao wataipataje
kwa vile harusi basi tena!
“Huku Dom (Dodoma)
hakukaliki bwana. Baadhi ya wabunge wameanza kuulizia michango yao, wanasema
kama harusi haipo basi na chao wakipate,” alisema mbunge mmoja akiomba
kuhifadhiwa jina.
Vicky Kamata akiwa katika pozi na mwanaume aliyepanga kuoana naye anayejulikana kwa jina la Charles wa jijini Dar. |
WABUNGE WATAJWA
KUINJINIA
Mbunge huyo
alikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa kuna wabunge wametajwa ‘kuinjia’ zengwe
la kutokufungwa kwa ndoa hiyo kwa sababu wanazozijua wao ambazo Ijumaa Wikienda
haikupewa lakini inaendelea kuzichimba.
VICKY KAMATA
Vicky alipotafuwa
kwa njia ya simu Jumamosi iliyopita ili azungumze lolote kuhusu kuyeyuka kwa
ndoa yake hakupatikana hewani.
CREDIT TO GROBAL
PUBLISHERS
No comments: